MACHAFUKO yalizuka katika bunge la Ghana Alhamisi usiku wa manane, huku wabunge wakiharibu samani, na kusukumana na kurushiana vijembe.
Machafuko yalianza baada ya wabunge
kutofautiana wakati wa kuwapiga msasa mawaziri wapya walioteuliwa na rais mpya
John Mahama – aliyechaguliwa Desemba 2024.
Kamati ya uhakiki ilikuwa
haikubaliani kuhusu masuala kadhaa, huku baadhi wakiwashutumu wabunge wa
upinzani kwa kuuondoa mchakato huo ili kusuluhisha matokeo ya kisiasa.
Siku ya Ijumaa asubuhi mwenyekiti wa
kamati ya uhakiki aliomba msamaha kwa umma wa Ghana, na kuitaja
"haikubaliki kabisa".
Kwa mujibu wa BBC, Kamati ya vyama
mbalimbali ilikuwa imeratibiwa kuwakagua wabunge watatu kutoka chama tawala cha
National Democratic Congress (NDC).
Watatu hao walikuwa wamependekezwa
kwa nyadhifa za uwaziri baada ya NDC kushinda chama cha New Patriotic Party
(NPP) katika uchaguzi wa Desemba.
Hata hivyo, wabunge wa NDC
walimshutumu Alexander Afenyo-Markin, kiongozi wa NPP bungeni, kwa kuwahoji
wateule wa mawaziri kwa muda mrefu bila sababu.
Zaidi ya saa tano zilitumika kumpiga
msasa mteule mmoja tu - waziri wa mawasiliano mteule Samuel Nartey George.
Wabunge wengi wa NDC wanaamini kuwa
hii ilikuwa ni aina ya malipo kutoka kwa wabunge wa upinzani kwenye kamati
hiyo, ambao walitaka George kubatilisha ukosoaji wake dhidi ya rais wa zamani
na kiongozi wa NPP Nana Akufo-Addo na Makamu wa Rais wa Akufo-Addo Mahamadu
Bawumia.
Wajumbe wa kamati ya uhakiki
waliishia kwa miguu - kupiga kelele, kusukumana na kurushiana vijembe na kuinua
meza.
Kutokana na hali hiyo, Spika wa bunge
aliwasimamisha kazi wabunge wanne - watatu kutoka NPP na mmoja wa chama tawala
- kwa wiki mbili.
Siku ya Ijumaa, Afenyo-Markin wa NPP
alisema desturi za bunge ziliruhusu wajumbe wa kamati "fursa ya kuchunguza
kwa kina kila aliyeteuliwa na rais, bila kikomo cha maswali".
Alishutumu NDC kwa kujaribu
"kukatisha tamaa" mchakato huu. Kutokana na fujo hizo, uhakiki huo
uliishia kuahirishwa hadi Ijumaa.
Uchaguzi mkuu ulifanyika mapema
Desemba mwaka jana ambapo rais wa zamani Rais wa zamani John Dramani Mahama alishinda
uchaguzi wa rais wa nchi hiyo baada ya mpinzani wake mkuu, Makamu wa Rais
Mahamudu Bawumia, kukubali kushindwa.
