RAIS William Ruto amewatolea pofu baadhi ya wanasiasa na wakenya wanaojaribu kukosoa sera zake.
Akizungumza katika kaunti ya Garissa wakati wa ziara yake ya
kimaendeleo katika eneo pana na Kaskazini Mashariki, kiongozi wa taifa alisema
kwamba yeye sit u kiongozi lakini pia ni msomi mwenye kitembo cha PhD.
Rais alisema kwamba baadhi ya watu wanaojaribu kukosoa sera
zake haswa mpango wa chanjo kwa mifugo ni wa elimu kidogo ambao hawana nafasi
ya kumshauri wala kumfundisha.
“Na mkiona wale
wanalalamika sijui wamesomea wapi. Si mimi niko na PhD? Si mimi naenewa nini
inaendelea Kenya? Sasa mimi Napata watu wengine wako na elimu kidogo kidogo
wanajaribu kunifundisha, mnanifundisha kazi gani?” rais alisema.
Kiongozi huyo aliwarai watu kutoka jamii za wafugaji katika
kaunti ya Garissa kutopinga mifugo wao kudungwa chanjo.
Kwa mujibu wa rais Ruto, Garissa ni kaunti ya pili kwa wingi
wa mifugo baada ya Turkana akisema kwamba wafugaji hao watanufaika na chanjo ya
bure ambayo inatolewa na serikali yake.
“Hii Garissa ndio kaunti
yenye iko na ng’ombe nyingi sana Kenya. Kenya hii ni ya 3 kwa wingi wa mifugo
barani Afrika n akaunti ambayo inaongoza ni Turkana ikifuatwa na hii ya Garissa….na
ndio sababu hiyo nimesema ile pesa mmekuwa mkitumia kwa chanjo ya ng’ombe sasa
serikali ya Kenya itawalipia.”
“Kama tunataka kuendesha
ukulima ili nyama yetu iwe na bei ya sawasawa, na maziwa yetu yauzwe katika
masoko ya Kenya na nje ya nchi, lazima tuwe taifa lililo huru kutokana na
magonjwa. Kama tuko na magonjwa kwa mifugo wetu tutakuwa wenyewe tunakwaza ile
soko ambayo tungepata kwa ajili ya mifugo yetu,” aliongeza.