logo

NOW ON AIR

Listen in Live

Mama akamatwa baada ya kumzika mtoto wake akiwa hai Makueni

Mtoto huyo mara moja alikimbizwa katika hospitali ya Sultan Hamud kwa matibabu.

image
na Tony Mballa

Habari09 February 2025 - 10:59

Muhtasari


  • Mama wa mtoto huyo amekamatwa na polisi na kwa sasa anazuiliwa katika Kituo cha Polisi cha Salama.
  • Anasubiri kufikishwa mahakamani kujibu mashtaka yanayohusiana na kifo cha mtoto huyo na kuzikwa kinyume cha sheria.

Mama akamatwa baada ya kumzika mtoto wake akiwa hai Makueni Mtoto wa siku moja alipatikana akiwa hai baada ya kuzikwa katika kijiji cha Kwa Nyunyi, Kaunti ya Makueni.

Mama wa mtoto huyo amekamatwa na polisi na kwa sasa anazuiliwa katika Kituo cha Polisi cha Salama.

Anasubiri kufikishwa mahakamani kujibu mashtaka yanayohusiana na kifo cha mtoto huyo na kuzikwa kinyume cha sheria.

Akizungumza na wanahabari baada ya tukio hilo, chifu msaidizi wa eneo hilo, Francis Kaluma, alisema aliamuru familia hiyo kuufukua mwili wa mtoto huyo baada ya kupokea kidokezo kutoka kwa majirani.

“Nilifahamishwa kuwa mwanamke alijifungua na kumzika mtoto wake akiwa hai. Nilienda pale na kutaka kujua mtoto alizikwa wapi. Walipoutoa mwili huo, tulishtuka kumpata mtoto huyo akiwa bado hai,” Kaluma alisema.

Mtoto huyo mara moja alikimbizwa katika hospitali ya Sultan Hamud kwa matibabu, lakini kwa masikitiko makubwa alifariki kutokana na majeraha na kuaga dunia Jumapili asubuhi.

Tukio hilo limeibua hofu katika jamii kwa wito wa kushughulikia kesi za kutelekezwa na unyanyasaji wa watoto.

Mamlaka za eneo hilo zimeapa kufuata haki kwa mtoto huyo huku zikiwataka wakaazi kuripoti shughuli zozote zinazotiliwa shaka kuhusu ustawi wa watoto.


RADIO JAMBO FREQUENCIES

Kisumu 100.1 | Mombasa 92.3 | Nakuru 96.9 | Eldoret 99.5 | Nyeri 99.3 | Nyahururu 97.3 | Webuye 95.3 | Meru 92.7 | Kitui 104.9 | Kibwezi 104.7 | Voi 105.7 | Malindi 98.1 | Lamu 104.7 | Narok 97.3 | Kapenguria 99.7 | Kisii 89.3 | Garissa 104.3 | Maralal 97.3 | Lodwar 92.7


logo© Radio Jambo 2024. All rights reserved