logo

NOW ON AIR

Listen in Live

Waititu akimbizwa hospitalini kutokana na shinikizo la damu

Haya yanajiri siku moja tu baada ya kuhukumiwa kifungo cha miaka 12 au kulipa faini ya Sh52.5 milioni.

image
na Tony Mballa

Habari14 February 2025 - 22:13

Muhtasari


  • Alishtakiwa pamoja na mkewe, Susan Ndung'u, ambaye alihukumiwa kifungo cha mwaka mmoja au kulipa faini ya Sh500,000.
  • Mahakama iliwatia hatiani kwa mashtaka yanayohusiana na ufisadi lakini ikawaachilia kwa makosa matatu ya utakatishaji fedha.

Aliyekuwa Gavana wa Kiambu Waititu amekimbizwa katika Hospitali ya Kitaifa ya Kenyatta (KNH) kutokana na matatizo ya shinikizo la damu.

Haya yanajiri siku moja tu baada ya kuhukumiwa kifungo cha miaka 12 au kulipa faini ya Sh52.5 milioni kufuatia kukutwa na hatia katika kesi ya ufisadi ya Sh588 milioni.

Katika hukumu hiyo katika Mahakama ya Milimani mnamo Alhamisi, Waititu vile vile alizuiwa kuwania kiti chochote cha kisiasa kwa kipindi cha miaka 7.

Alishtakiwa pamoja na mkewe, Susan Ndung'u, ambaye alihukumiwa kifungo cha mwaka mmoja au kulipa faini ya Sh500,000.

Mahakama iliwatia hatiani kwa mashtaka yanayohusiana na ufisadi lakini ikawaachilia kwa makosa matatu ya utakatishaji fedha.

Mshtakiwa mwenzao, mkurugenzi wa Testimony Enterprises Limited Charles Chege, pia amepigwa faini ya Sh295 milioni au kutumikia kifungo cha miaka 9 jela.

Beth Wangeci, mkurugenzi wa pili katika Testimony Enterprises Limited pia alitozwa faini ya Ksh.1 milioni au kutumikia kifungo cha mwaka mmoja jela.

Maarufu Zaidi

RADIO JAMBO FREQUENCIES

Kisumu 100.1 | Mombasa 92.3 | Nakuru 96.9 | Eldoret 99.5 | Nyeri 99.3 | Nyahururu 97.3 | Webuye 95.3 | Meru 92.7 | Kitui 104.9 | Kibwezi 104.7 | Voi 105.7 | Malindi 98.1 | Lamu 104.7 | Narok 97.3 | Kapenguria 99.7 | Kisii 89.3 | Garissa 104.3 | Maralal 97.3 | Lodwar 92.7


logo© Radio Jambo 2026. All rights reserved