Mama huyo amefichua kwamba amefikia maamuzi hayo baada watoto wake hao ambao ni wa kiume kuendelea kudhofika kiafya baada ya kuathirika kutokana na matumizi ya dawa za kulevya.
Philomena Alimo mwenye umuri wa miaka 45, ameeleza kwamba ndoa yake ilisambaratika miaka 13, na watoto wake ndio walikua wamebaki kama matumaini ila pia wameamua kuingilia mihadharati.
"Mimi kama mama ya watoto hao wawili, nilipoona hao vijana wakiwa wameharibika hivyo na maisha yao ya hapo mbeleni hakuna matumaini. Nimeamua kuuza figo zangu mbili, moja ya mtoto wangu wa kwanza na nyingine ya mtoto wangu wa pili," alieleza mwanamke huyo.
Nimeishi maisha yangu na sioni haja ya kuishi wakati watoto wangu wwanaangamia. Ndiposa nimechukua hii hatua na nimeamua kuuza figo zote mbili,' aliendelea.
Mama huyo wa watoto wawili ameeleza kwamba aliamua kuchukua maamuzi hayo baada ya juhudi zake za kutafuta usaidi kutoka kwa watu tofauti tofauti na ofisi mbalimbali kugonga mwamba.
"Kabla hata sijachukua hii hatua, nimezunguka kwote nikitafuta msaada ili vijana wangu hao wawili waweze kusaidiwa na wapelekwe katika madaktari wa kuwasaidia,' alisema.
Nimeenda kwa maaskofu, wachungaji, serikali, nimeenda kwa advocates ili kuuliza namna ya kuweza kusaidia hawa vijana. Nimetembelea jamii, nimeuliza marafiki lakini sijaweza kupata msaada,' aliweka wazi Alimo.
Mama huyo ambaye alizungumza kwa uchungu amesisitiza kwamba yuko tayari kuyapoteza maisha yake ila watoto wake wasaidiwe kurejelea hali yao ya awali.
'Najua ni maamuzi magumu ambaye nimechukua, lakini sioni ubaya kupoteza maisha yangu kwa ajili ya watoto wangu," Mwanamke huyo alisimulia kwa uchungu.