

RAIS wa Uganda, Yoweri Museveni ameonekana kughadhabishwa na utafiti mpya unaofanywa na watafiti katika chuo kikuu cha Makerere ambao wanafumbua njia mpya ya kuongeza lishe ya nyama na Samaki kwenye vyakula vya ng’ombe.
Wakati wa uzinduzi wa Wiki ya Utafiti na
Ubunifu mwaka huu katika chuo hicho kikuu, Museveni alitambulishwa kwa mradi
unaohusisha samaki na nyama kwenye chakula cha ng'ombe.
Rais huyo ambaye ni mfugaji wa ng’ombe
wengi alikuwa wa haraka kuonyesha mashaka yake katika utafiti huo, akisema
kwamba unapotosha kutoka tamaduni za tangu jadi za kulisha ng’ombe nyasi na
majani tu.
“Nimeona tu kwenye vibanda watu
wanatengeneza vyakula vya mifugo. Niliona kwamba wanawafanya ng'ombe kula
samaki ... kwamba malisho ya ng'ombe yana samaki na nyama.”
Kulingana na Museveni, ni vizuri ng’ombe
kusalia katika kulishwa nyasi na majani tu kwa sababu Samadi yao hutumiwa
katika kuboma nyumba za matope na ikifikia wanalishwa nyama kama binadamu, basi
kinyesi chao kitakuwa kinanuka kisiweze kutumika tena katika shughuli kama hizo
na binadamu.
“Katika Ankole, kinyesi cha binadamu
kina jina, na kinanuka sana kwa sababu ya kile ambacho wanadamu hula. Tunakula
nafaka, nyama n.k. Ng'ombe, kwa upande mwingine, wana jina la kinyesi chao,
ambacho hakina harufu; hata tunaishughulikia na kuitumia kupamba nyumba zetu. “
“Lakini sasa naanza kuwa na wasiwasi.
Ikiwa ng'ombe anakula chakula cha binadamu, bado hutoa kinyesi chake cha asili?” Museveni alihoji.
Alihoji zaidi ikiwa mfumo wa mmeng'enyo wa
ng'ombe, ambao ni wanyama wanaokula mimea, unaweza hata kushughulikia lishe
kama hiyo.
“Kuku na nguruwe wanaweza kulishwa
kwa nyama kwa sababu hata kwa asili wanaweza kuishughulikia, lakini ng'ombe,
mbuzi na kondoo, tunahitaji kutafuta njia zingine ambazo hazihusishi kuwalisha
kwa nyama.”
Rais alipendekeza kuwa ingawa sayansi
inaweza kutoa fursa mpya, baadhi ya mazoea yanapaswa kuchukuliwa kuwa
"mwiko" na kukataliwa, haswa wakati yanatatiza mifumo asilia.