logo

NOW ON AIR

Listen in Live

Matiang’i Ataka Polisi Wakome Kutumia Silaha Dhidi ya Waandamanaji

Aliwataka Wakenya wa mitazamo yote ya kisiasa kuweka kando tofauti zao na kushikamana kupigania ukombozi wa nchi .

image
na Tony Mballa

Habari25 June 2025 - 19:04

Muhtasari


  • Matiang’i alitoa matamshi hayo kufuatia ripoti kwamba angalau watu saba waliuawa na wengine wengi kujeruhiwa wakati wa maandamano ya Jumatano yaliyofanyika kuwaenzi waandamanaji wa kizazi cha Gen Z waliouawa kwa kupigwa risasi na polisi mwaka uliopita.
  • Waandamanaji hao walikuwa miongoni mwa wale waliokuwa wakieleza wasiwasi wao kuhusu Mswada wa Fedha wa 2024, sera kandamizi za ushuru, usimamizi mbaya wa rasilimali za umma, kupunguzwa kwa ufadhili wa serikali kwa vyuo vikuu, na masuala mapana ya utawala.

Waziri wa zamani wa Usalama wa Ndani, Dkt. Fred Matiang’i, amelaani hatua ya polisi kutumia nguvu dhidi ya waandamanaji.

Matiang’i alitoa matamshi hayo kufuatia ripoti kwamba angalau watu saba waliuawa na wengine wengi kujeruhiwa wakati wa maandamano ya Jumatano yaliyofanyika kuwaenzi waandamanaji wa kizazi cha Gen Z waliouawa kwa kupigwa risasi na polisi mwaka uliopita.

Waandamanaji hao walikuwa miongoni mwa wale waliokuwa wakieleza wasiwasi wao kuhusu Mswada wa Fedha wa 2024, sera kandamizi za ushuru, usimamizi mbaya wa rasilimali za umma, kupunguzwa kwa ufadhili wa serikali kwa vyuo vikuu, na masuala mapana ya utawala.

Maafisa wa polisi wakishika doria

“Katika kufanya hivyo, hawa raia vijana waliokuwa na ari walikuwa wakitumia haki yao ya kikatiba ya kuwasilisha malalamiko yao kwa mamlaka. Ninaunga mkono kikamilifu hisia walizotoa. Naishauri serikali isifumbe moyo wake bali isikilize kwa dhati kilio cha wananchi kuhusu haki na mageuzi,” alisema Matiang’i.

“Matumizi ya nguvu na mamlaka yatazidisha tu mgogoro na kuiweka nchi kwenye mwelekeo wa hatari na wa utelezi. Pole zangu za dhati ziende kwa familia zilizopoteza wapendwa wao katika kipindi cha mwaka mmoja uliopita chini ya hali hizi za kusikitisha,” alisema Matiang’i.

Aliwataka Wakenya wa mitazamo yote ya kisiasa kuweka kando tofauti zao na kushikamana kupigania ukombozi wa nchi dhidi ya uongozi wa kifisadi.

Maafisa wa polisi waliotumwa kukabiliana na waandamanaji

“Lazima tuungane kuvuka mipaka ya vyama vya siasa na vizazi, kurekebisha yaliyoharibika na kujenga mustakabali wa haki, uwajibikaji na ushirikishwaji wa wote.”

Aliwahimiza polisi kuwa na kiasi wanapokabiliana na waandamanaji.

“Pia ninatoa ombi la dhati kwa maafisa wetu wa usalama: tafadhali msielekeze silaha zenu kwa wananchi wenzenu. Kuweni na kiasi na busara. Msikabiliane na maandamano ya amani kwa kutumia nguvu.”

“Ni kupitia tu mazungumzo na utayari wa kweli wa kusikiliza ndipo tutakapoweza kupata njia ya kusuluhisha malalamiko kwa amani na kurejesha utulivu katika taifa letu tunalolipenda.”

Waandamanaji

Makala Zinazohusiana


RADIO JAMBO FREQUENCIES

Kisumu 100.1 | Mombasa 92.3 | Nakuru 96.9 | Eldoret 99.5 | Nyeri 99.3 | Nyahururu 97.3 | Webuye 95.3 | Meru 92.7 | Kitui 104.9 | Kibwezi 104.7 | Voi 105.7 | Malindi 98.1 | Lamu 104.7 | Narok 97.3 | Kapenguria 99.7 | Kisii 89.3 | Garissa 104.3 | Maralal 97.3 | Lodwar 92.7


logo© Radio Jambo 2024. All rights reserved