logo

NOW ON AIR

Listen in Live

Ruto Aapa Kuunganisha Kenya Akisaidiwa Na Raila

Ruto alisema hayo katika kaunti ya Kilifi ambako alihudhuria mazishi ya baba yake Gavana wa Kilifi, Gideon Mung’aro.

image
na Tony Mballa

Habari25 June 2025 - 17:00

Muhtasari


  • Wakati hisia zilikuwa juu na miito mipya ya kutafuta haki ikisikika kote nchini, uwepo wa kimya wa Ruto huko Kilifi uliibua maswali, hata wakati serikali iliendelea kushikilia msimamo mkali dhidi ya waandamanaji.
  • Maadhimisho ya kumbukumbu ya Jumatano yaliandamwa na uwepo mkubwa wa polisi, visa vya vurugu vya hapa na pale, na ukandamizaji wa vyombo vya habari, lakini pia yaligubikwa na nyakati za mshikamano na amani miongoni mwa waandamanaji wanaoongozwa na kizazi cha Gen Z.

Rais William Ruto ameapa kuunganisha taifa akisaidiwa na viongozi wengine akuwemo kinara wa ODM Raila Odinga.

"Nitafanya bidii kama kiongozi wa taifa hili, nikisaidiwa na Baba na viongozi wengine, tutaunganisha taifa letu la Kenya kuwe ni mahali hakuna chuki na ukablia," Ruto alisema.

Ruto alisema hayo katika kaunti ya Kilifi ambako alihudhuria mazishi ya baba yake Gavana wa Kilifi, Gideon Mung’aro.

"Rambirambi zetu kwa Gavana Gideon Mung’aro kufuatia kifo cha baba yake, Mzee Gideon Mung’aro Senior. Alikuwa kiongozi anayeheshimika, wa maendeleo na mchapakazi," alisema Ruto.

"Familia, marafiki na watu wa Kilifi wako katika maombi yetu wakati huu wa majonzi," aliongeza.

Kiongozi wa nchi aliandamana na washirika wake wakuu wa serikali akiwemo Spika wa Seneti Amason Kingi, na Waziri Mkuu wa zamani Raila Odinga, ambaye sasa anaonekana kama mshirika muhimu katika mpangilio wa serikali jumuishi ya Ruto.

Rais Ruto siku ya Jumanne aliwatetea polisi, akiwataka kuchukua hatua kali dhidi ya kile alichokitaja kama kutotii sheria za kiraia, hata wakati makundi ya kutetea haki za binadamu na mabalozi walionya dhidi ya matumizi ya nguvu kupita kiasi.

Kutokuwepo kwake jijini wakati wa siku ya mvutano mkubwa kitaifa na ya kukumbuka waliopoteza maisha hakukupita bila kuonekana, hasa wakati Wakenya wengi walijitokeza kuwaenzi zaidi ya watu 60 waliopoteza maisha yao wakati wa maandamano ya kupinga Mswada wa Fedha mwaka jana, yaliyokamilika kwa waandamanaji kuvamia Bunge.

Wakati hisia zilikuwa juu na miito mipya ya kutafuta haki ikisikika kote nchini, uwepo wa kimya wa Ruto huko Kilifi uliibua maswali, hata wakati serikali iliendelea kushikilia msimamo mkali dhidi ya waandamanaji.

Maadhimisho ya kumbukumbu ya Jumatano yaliandamwa na uwepo mkubwa wa polisi, visa vya vurugu vya hapa na pale, na ukandamizaji wa vyombo vya habari, lakini pia yaligubikwa na nyakati za mshikamano na amani miongoni mwa waandamanaji wanaoongozwa na kizazi cha Gen Z.

Makala Zinazohusiana


RADIO JAMBO FREQUENCIES

Kisumu 100.1 | Mombasa 92.3 | Nakuru 96.9 | Eldoret 99.5 | Nyeri 99.3 | Nyahururu 97.3 | Webuye 95.3 | Meru 92.7 | Kitui 104.9 | Kibwezi 104.7 | Voi 105.7 | Malindi 98.1 | Lamu 104.7 | Narok 97.3 | Kapenguria 99.7 | Kisii 89.3 | Garissa 104.3 | Maralal 97.3 | Lodwar 92.7


logo© Radio Jambo 2024. All rights reserved