logo

NOW ON AIR

Listen in Live

Bintiye Moody Awori, Maria aaga dunia

Maria Abadiou, Binti mdogo wa naibu rais wa zamani, Moody Awori ameaga dunia.

image
na Radio Jambo

Habari07 June 2023 - 12:26

Muhtasari


•Familia ya Awori ilithibitisha habari hizo za kuvunja moyo siku ya Jumatano ambapo ilithibitishwa aliaga mwendo wa asubuhi.

Maria Abadiou Awori, Binti mdogo wa makamu rais wa zamani, Moody Awori ameaga dunia.

Familia ya Awori ilitangaza habari hizo za kuvunja moyo siku ya Jumatano mchana ambapo ilithibitishwa aliaga mwendo wa asubuhi.

"Alianguka jana usiku na kukimbizwa katika Hospitali ya Nairobi ambapo Madaktari walimpatia matibabu ya dharura katika jitihada za kuokoa maisha yake lakini haikusaidia. Hospitali ilitangaza asubuhi kwamba amefariki," taarifa kutoka kwa familia ambayo ilifikia Radio Jambo ilisoma.

Spika Amason Kingi alithibitisha kifo cha Marya katika seneti,

"Ni kwa masikitiko makubwa ninawaarifu kuhusu kufariki kwa Bi Marya Elizabeth Adjibodou, Karani Mkuu Msaidizi wa Kwanza, akihudumu katika  idara ya Huduma za Sheria na Taratibu katika Seneti," Kingi alitangaza.

Kingi hata hivyo hakufichua sababu ya kifo cha Maria.

Seneta wa Kakamega Boni Khalwale alimuomboleza Marya,"Pole zangu maalum kwa mjomba Moody na familia yake.  Enda vyema dada yangu."

Maria ni mke wa Mike Abadiou.

Marehemu alikuwa na shahada ya uzamili na shahada ya kwanza kutoka Chuo cha New Hampshire, jijini Manchester, nchini Uingereza.


RADIO JAMBO FREQUENCIES

Kisumu 100.1 | Mombasa 92.3 | Nakuru 96.9 | Eldoret 99.5 | Nyeri 99.3 | Nyahururu 97.3 | Webuye 95.3 | Meru 92.7 | Kitui 104.9 | Kibwezi 104.7 | Voi 105.7 | Malindi 98.1 | Lamu 104.7 | Narok 97.3 | Kapenguria 99.7 | Kisii 89.3 | Garissa 104.3 | Maralal 97.3 | Lodwar 92.7


logo© Radio Jambo 2024. All rights reserved