logo

NOW ON AIR

Listen in Live

Hisia mseto baada ya Eddie Butita kutangaza anatarajia mtoto na mpenzi wake

Mchekeshaji huyo alidokeza kwamba anafurahi sana kuhusu ujauzito huo.

image
na Radio Jambo

Habari28 October 2022 - 04:29

Muhtasari


•Butita alichapisha video iliyoonyesha akimpapasa mjamzito na kuambatanisha na ujumbe ulioashiria kuwa ni mtoto wake aliyebebwa tumboni.

•Wanamitandao Wakenya wakiwemo watu kadhaa mashuhuri walikuwa wepesi kumpongeza mchekeshaji huyo kwa hatua hiyo kubwa.

Mchekeshaji na mwandishi mashuhuri Eddie Butita amedokeza kuwa huenda akaitwa baba hivi karibuni.

Alhamisi, mchekeshaji huyo wa zamani wa Churchill Show alichapisha video iliyoonyesha akimpapasa mjamzito na kuambatanisha na ujumbe ulioashiria kuwa ni mtoto wake aliyebebwa tumboni.

"Ni mvulana au ni msichana? Jumatatu 9.00AM #TheGrandGenderReveal," aliandika kwenye video hiyo.

Butita aliambatanisha video hiyo na wimbo wa Nadia Mukami na Arrow Bwoy 'Kai Wangu' ambao walimwimbia mtoto wao.

Katika maelezo ya video hiyo, mchekeshaji huyo alidokeza kwamba anafurahi sana kuhusu ujauzito huo.

"Hakuna maneno yanaweza kuelezea hili, 2 imekuwa nambari yangu ya bahati kila wakati na 2022 ina mbili tatu. Ni mvulana au msichana? Tuonane Jumatatu," aliandika.

Hata kabla ya madai ya Butita kuthibitishwa kuwa kweli ama kiki tu, Wanamitandao Wakenya wakiwemo watu kadhaa mashuhuri walikuwa wepesi kumpongeza mchekeshaji huyo kwa hatua hiyo kubwa.

Hata hivyo, baadhi walieleza mashaka yao kuhusu madai ya msanii huyo na kusema kwamba alikuwa akiigiza tu.

Blessednjugush: Hongera kwa booties

jackyvike: Ala ulienda kugawa nyota, nyota nayo ikagawana, kongole

ogaobinna: Hiyo ni tumbo ya dem ya wenyewe unashika hivyo

mcatricky: We wacha kutuenjoy

celestinendinda: Hongera kwa Butitas

dj shiti_comedian: Pongezi sana CEO

Kwa muda mrefu Butita amejaribu kuweka mahusiano yake kuwa siri.

Hata hivyo, kwa miaka mingi imekuwa ikidaiwa kuwa anachumbiana na mchekeshaji mwenzake Eunice Mammito, madai ambayo wote wawili wamewahi kuyazungumzia hapo awali kwa mafumbo.


RADIO JAMBO FREQUENCIES

Kisumu 100.1 | Mombasa 92.3 | Nakuru 96.9 | Eldoret 99.5 | Nyeri 99.3 | Nyahururu 97.3 | Webuye 95.3 | Meru 92.7 | Kitui 104.9 | Kibwezi 104.7 | Voi 105.7 | Malindi 98.1 | Lamu 104.7 | Narok 97.3 | Kapenguria 99.7 | Kisii 89.3 | Garissa 104.3 | Maralal 97.3 | Lodwar 92.7


logo© Radio Jambo 2024. All rights reserved