logo

NOW ON AIR

Listen in Live

Hisia mseto baada ya Guardian Angel kuonekana ameweka mikono kwenye matiti ya Esther Musila, wakosoaji wajibiwa (+picha)

Bi Musila ambaye alionekana kutofurahishwa na maoni hayo alijibu kwa ukali, “Kuna matiti yako imepotea ama imeshikwa inakuuma?”

image
na Radio Jambo

Habari30 September 2023 - 10:47

Muhtasari


•Guardian Angel alionekana akiwa amesimama nyuma ya mhasibu huyo mwenye umri wa miaka 53  na kunyoosha mkono wake wa kushoto na kuulaza kwenye titi lake.

•Bi Musila ambaye alionekana kutofurahishwa na maoni hayo alijibu kwa ukali, “Kuna matiti yako imepotea ama imeshikwa inakuuma?”

Wanandoa mashuhuri Peter Omwaka almaarufu Guardian Angel na Esther Musila wameendelea kusherehekeana hadharani na kuonyesha mapenzi yao mazito.

Wanandoa hao mara nyingi hupostiana kwenye mitandao yao ya kijamii na kuandikiana jumbe tamu, ishara tosha kuwa wamefurahishwa sana na ndoa yao. Licha ya wengi kuwafurahia na kuwasherehekea, hawajakosa wenye chuki na wakosoaji ambao hutoa maoni hasi kwenye machapisho yao ya mitandao ya kijamii.

Siku ya Jumamosi asubuhi, Bi Musila alishiriki picha nzuri zake na mumewe wakifurahia wakati pamoja nyumbani kwao.

"Siku itakuwa nzuri tu kama mawazo uliyonayo ..." Musila aliandika chini ya picha hizo.

Katika picha hizo ya selfie, Guardian Angel alionekana akiwa amesimama nyuma ya mama huyo wa watoto watatu wakubwa na kunyoosha mikono yake na kuilaza kwenye titi lake la kushoto na la kulia kwenye picha tofauti. Wawili hao walionekana kuwa na furaha pamoja na tabasamu kubwa zuri lilijaza nyuso zao.

Chapisho hilo hata hivyo lilikaribisha ukosoaji mwingi kutoka kwa kundi la watumiaji wa mtandao ambao walihisi kuwa tabia iliyoonyeshwa kwenye picha haikuwa ya maadili.

@zuri_collections254 alisema, “Sasa umeanza kuwa na tabia za amber ray na rapudo. Matiti lazima ishikwe?"

Bi Musila ambaye alionekana kutofurahishwa na maoni hayo alijibu kwa ukali, “Kuna matiti yako imepotea ama imeshikwa inakuuma?”

Mkosoaji mwingine, @roba_49 alisema "Ben 10 na mumama wake."

Alijibu, "Kabisa, utafanya?"

Mwanamitandao mwingine alitoa maoni yake akisema, “Huyu haogopi laana” na mhasibu huyo mwenye umri wa miaka 53 akajibu “Kwenyu kama laana inakusumbua ugua pole. Haituhusu.”

Hata hivyo, sio kila mtu aliyetoa maoni alikosoa wanandoa hao kwani wengine walitoa maneno ya fadhili na kuwatetea dhidi ya ukosoaji.

@perisetieno alisema “When Jesus say yes nobody can say no.. aki nyinyi watu hamujawahi kuchoka, si ni husband and wife wako na right to touch anywhere, sasa hiyo ni kuguzwa tu, na akipost guardian akinyonya. Si mtafadhaika."

Bi Musila alionekana kukubaliana na maneno ya shabiki huyo akisema "hawatawahi kuamka."

@look_empire_254 alisema “Nawapenda wanandoa hawa. Wazuri na wenye joto.”

Esther Musila na Guardian Angel wamekuwa katika uhusiano thabiti  kwa miaka mitatu iliyopita na walifanya ndoa yao rasmi kwa kufunga pingu za maisha mapema  mwaka jana. Mara nyingi wamekuwa wakikosolewa hasa kutokana na tofauti zao kubwa za umri lakini hilo halijawazuia na badala yake wanaonekana kuimarika pamoja siku hadi siku.


RADIO JAMBO FREQUENCIES

Kisumu 100.1 | Mombasa 92.3 | Nakuru 96.9 | Eldoret 99.5 | Nyeri 99.3 | Nyahururu 97.3 | Webuye 95.3 | Meru 92.7 | Kitui 104.9 | Kibwezi 104.7 | Voi 105.7 | Malindi 98.1 | Lamu 104.7 | Narok 97.3 | Kapenguria 99.7 | Kisii 89.3 | Garissa 104.3 | Maralal 97.3 | Lodwar 92.7


logo© Radio Jambo 2024. All rights reserved