logo

NOW ON AIR

Listen in Live

Watoto 25 wafariki baada ya darasa lao kuungua moto Niger

Moto uliotokea Jumatatu umeteketeza madarasa matatu , meya wa mji Maradi, Chaibou Aboubacar, ameviambia vyombo vya habari.

image
na Radio Jambo

Kimataifa09 November 2021 - 04:47

Muhtasari


• Watoto wapatao 25 wenye umri kati ya miaka mitano na sita wamefariki baada ya darasa lao kuungua moto.

• Chanzo cha moto huo bado hakijafahamika bado.

• Masomo yamesitishwa katika shule hiyo kwa muda.

Watoto wapatao 25 wenye umri kati ya miaka mitano na sita wamefariki baada ya darasa lao kuungua moto.

Wengine kadhaa walijeruhiwa wakati wa ajali hiyo ya moto ambayo ilitokea Jumatatu asubuhi wakati watoto wakiwa darasani wakisoma katika shule iliyopo eneo la Maradi.

Chanzo cha moto huo bado hakijafahamika bado.

Nchini Niger, madarasa huwa yanajaa na mara nyingi hujengwa kwa kutumia mbao na majani wakati miundo mikuu ya matofali haiwezi kujenga shule zote.

Moto uliotokea Jumatatu umeteketeza madarasa matatu, meya wa mji wa Maradi, Chaibou Aboubacar, ameviambia vyombo vya habari.

Shuhuda mmoja ameiambia BBC kuwa ameona watoto kadhaa wakitolewa eneo la tukio na kupelekwa hospitali wakiwa katika hali ya mahututi.

Masomo yamesitishwa katika shule hiyo kwa muda.

Si kawaida kwa shule za Niger kuungua na kusababisha idadi kubwa ya vifo.

Ingawa mwanzoni mwa mwaka huu katika mji mkuu wa nchi hiyo shule iliungua na kuua watoto 20 .


RADIO JAMBO FREQUENCIES

Kisumu 100.1 | Mombasa 92.3 | Nakuru 96.9 | Eldoret 99.5 | Nyeri 99.3 | Nyahururu 97.3 | Webuye 95.3 | Meru 92.7 | Kitui 104.9 | Kibwezi 104.7 | Voi 105.7 | Malindi 98.1 | Lamu 104.7 | Narok 97.3 | Kapenguria 99.7 | Kisii 89.3 | Garissa 104.3 | Maralal 97.3 | Lodwar 92.7


logo© Radio Jambo 2024. All rights reserved