Shirika la Afya Ulimwenguni (WHO) limethibitisha kwamba Misri haina malaria - jambo ambalo shirika la afya ya umma la Umoja wa Mataifa lilisema ni "la kihistoria".
"Malaria ni ya zamani kama ustaarabu wa Misri yenyewe, lakini ugonjwa ambao uliwasumbua mafarao sasa ni historia," mkuu wa WHO Tedros Adhanom Ghebreyesus alisema.
Mamlaka ya Misri ilizindua juhudi zao za kwanza kukomesha ugonjwa hatari wa kuambukiza unaoenezwa na mbu karibu miaka 100.
Uidhinishaji hutolewa wakati nchi inapothibitisha kuwa mkondo wa usambazaji umekatizwa kwa angalau miaka mitatu mfululizo iliyopita.
Malaria huua watu wasiopungua 600,000 kila mwaka, karibu wote ni kutoka barani Afrika.