Polisi katika taifa la Msuimbiji waliuwa takriban watu 11 na kusababisha majeraha kwa wengine zaidi ya 50 baada ya mfarakano wa matokeo ya kiti cha urais nchini humo.
Taarifa hizi zilithibitishwa na makundi ya kutetea haki za kibanadamu nchini humo.
Maandamano yalianzishwa mnamo tarehe 29 Oktoba na kufuatisha mauaji ya watu hao.
Maandamano hayo yalisababishwa na kutawazwa kwa Daniel Chapo ambaye ni kiongozi wa chama cha Frelimo ambacho kimekuwa kikitawala tangia 1975.
Daniel Chapo alitawazwa mshindi wa kiti cha Urais kwa kura ambazo zilipigwa mnamo tarehe 9 Oktoba.
Ni jambo ambalo lilifuatisha mfarakano mkali baina ya wananchi na polisi.Wananchi hawa ambao kwa wingi ni wale wa upinzani walijaza mitaa na mabango wakiandamana.
Kundi la kibinadamu la HRW lilisema kuwa watu zaidi ya 50 walipata majeraha mabaya ya risasi huku wengine wakiwa hali mahututi kufikia sasa.
Vile vile kundi hilo lilisema kuwa watoto wadogo wa chini akiwa wa mwaka mmoja walivuta hewa ya vitoa machozi baada ya polisi kuvirusha bila mipangilio.
Allan Ngari, ambaye ni katibu msemaji wa kundi hilo la haki za kibinadamu, alisema kuwa serikli ya taifa hilo yafaa kuchunguza utumizi mbaya wa nguvu kupita kiasi.
Katika maandamano hayo, watu zaidi ya 450 walitiwa mbaroni wengi wakitiwa katika mji mkuu wa taifa hilo Maputo.
Tume ya uchaguzi ya Musumbiji ilitoa taarifa na kusema kuwa Chapo alitwaa nafasi ya kwanza ya Urais kwa asilimia 71 huku mpinzani wake wa chama pinzani Venancio Mondlane akifanikiwa kupata asilimia 20 ya kura.
Kwa matokeo hayo sasa chama cha Venancio Mondlane cha Podemos kinata shughli ya kuhesabu kura irejelewe tena