logo

NOW ON AIR

Listen in Live

Washukiwa wa kundi la madhehebu ya kidini waua 10 Uganda

Takribani watu 10 wamethibitishwa kufariki,na wengine 8 wamelazwa hospitali.

image
na BBC NEWS

Kimataifa31 October 2024 - 15:20

Muhtasari


  • Kwa mujibu wa Meja Katamba Jeshi la Uganda na Polisi wameanza msako kuwabaini washukiwa wa shambulizi hilo wakati uchunguzi unaendelea.




Polisi walisema washukiwa wawili pia waliuawa walipokuwa wakijaribu kushambulia vikosi vya usalama.

Takribani watu 10 wamethibitishwa kufariki,na wengine 8 wamelazwa hospitali baada ya kujeruhiwa katika shambulizi lililotekelezwa katika Wilaya ya Kigadi,Magharibi mwa Uganda,

Polisi na Jeshi la Uganda UPDF lilithibitisha jumatano.

‘’Taarifa za awali zinaonesha kwamba wanakikundi cha madhehebu ya kidini,ambacho jina lake halijafahamika walishambulia familia ambazo wengi wao ni jamaa zao kwa kuwakata kwa kifaa chenye ncha kali na kusababisha vifo na majeruhi’’alieleza Mejaj Bilal Katamba baada ya shambulizi la saa tatu usiku katika Kijiji cha Muzizi.

Kwa mujibu wa Meja Katamba Jeshi la Uganda na Polisi wameanza msako kuwabaini washukiwa wa shambulizi hilo wakati uchunguzi unaendelea.

Katika taarifa nyingine,msemaji wa polisi katika mkoa wa Albertine SP Julius Allan Hakiza aliwataja waliouawa miongoni mwao Watoto wanne.

‘’Wengine 8 wamelazwa katika vituo vya afya huko Kyaterekera.Jopo la maafisa polisi likiongozwa na DPC Kagadi Ampurira Kenneth na maafisa wa Jeshi,wanashughulikia tukio hilo.

‘’Tunachunguza tukio hili,na sababu za shambulizi hili ambazo bado hazijafahamika.Tunaisihi jamii kutoa taarifa zozote zinazohusiana na tukio hili.Ushirikiano wenu ni muhimu ili kuwafikisha wahusika mbele ya sheria’’SP Hakiza aliongeza



RADIO JAMBO FREQUENCIES

Kisumu 100.1 | Mombasa 92.3 | Nakuru 96.9 | Eldoret 99.5 | Nyeri 99.3 | Nyahururu 97.3 | Webuye 95.3 | Meru 92.7 | Kitui 104.9 | Kibwezi 104.7 | Voi 105.7 | Malindi 98.1 | Lamu 104.7 | Narok 97.3 | Kapenguria 99.7 | Kisii 89.3 | Garissa 104.3 | Maralal 97.3 | Lodwar 92.7


logo© Radio Jambo 2024. All rights reserved