logo

NOW ON AIR

Listen in Live

Mpaka wa Rwanda na DR Congo waripotiwa kufungwa

Mpaka kati ya DR Congo na Rwanda umeripotiwa kufungwa baada ya waasi wa M23 kuingia Goma.

image
na BBC NEWS

Kimataifa27 January 2025 - 15:14

Muhtasari


  • Chanzo cha kidiplomasia na mashahidi waliliambia shirika la habari la AFP kwamba hakuna mtu anayeruhusiwa kuingia au kutoka kwenye kivuko kikuu kati ya nchi hizo mbili.
  • Kundi la M23 liliichukua udhibiti wa mji wa Goma kwa muda mfupi wakati wa uasi mwaka 2012, lakini wakajiondoa baada ya makubaliano ya amani kufikiwa.


Mpaka kati ya DR Congo na Rwanda umeripotiwa kufungwa baada ya waasi wa M23 kuingia Goma.

Chanzo cha kidiplomasia na mashahidi waliliambia shirika la habari la AFP kwamba hakuna mtu anayeruhusiwa kuingia au kutoka kwenye kivuko kikuu kati ya nchi hizo mbili.

Ni wafanyikazi wasio wa lazima tu wa Umoja wa Mataifa na familia zao waliruhusiwa kuvuka walipokuwa wakihamishwa kupitia Rwanda.

Shirika la utangazaji la serikali ya Rwanda liliripoti kuwa baadhi ya mabasi yalikuwa yasubiri kuwahamisha wafanyakazi na familia za Umoja wa Mataifa.

Goma iko wapi na kwa nini ni muhimu?

Goma ni mji mkuu wa eneo la Kivu Kaskazini na nyumbani kwa zaidi ya watu milioni moja. Mji hio ambao uko kwenye mpaka wa DRC na Rwanda ni kitovu muhimu cha biashara na usafirishaji ambacho kinaunganisha miji ya uchimbaji madini inayosambaza madini na madini yanayohitajika sana, kama vile dhahabu, bati na coltan, kiungo muhimu katika utengenezaji wa simu za mkononi.

Kundi la M23 liliichukua udhibiti wa mji wa Goma kwa muda mfupi wakati wa uasi mwaka 2012, lakini wakajiondoa baada ya makubaliano ya amani kufikiwa.



RADIO JAMBO FREQUENCIES

Kisumu 100.1 | Mombasa 92.3 | Nakuru 96.9 | Eldoret 99.5 | Nyeri 99.3 | Nyahururu 97.3 | Webuye 95.3 | Meru 92.7 | Kitui 104.9 | Kibwezi 104.7 | Voi 105.7 | Malindi 98.1 | Lamu 104.7 | Narok 97.3 | Kapenguria 99.7 | Kisii 89.3 | Garissa 104.3 | Maralal 97.3 | Lodwar 92.7


logo© Radio Jambo 2024. All rights reserved