Aliyekuwa Rais wa Marekani Joe Biden amekosoa sera za ustawi wa jamii katika utawala wa Trump kwenye hotuba yake ya kwanza tangu kuondoka madarakani.
Rais huyo wa zamani wa Marekani aliuambia mkutano huko Chicago kwamba serikali imechukua "mwelekeo wa kikatili" katika Idara ya Ustawi wa Jamii, mfumo ambao Donald Trump na Elon Musk - ambaye anaongoza juhudi za kupunguza gharama za Ikulu ya White House - wamesema umekumbwa na udanganyifu.
Biden hakumtaja Trump kwa jina wakati wa hotuba yake siku ya Jumanne, lakini alisema: "Katika muda usiozidi siku 100, utawala huu mpya umefanya uharibifu mkubwa na mabaya mengi. Ni jambo la kusikitisha"
Biden - ambaye alikuwa akizungumza katika hafla ya haki za walemavu - hakugusia kuondoka kwake kutoka Ikulu ya White au uchaguzi wa rais wa 2024.
Wanasiasa wa chama cha Democratic wameushutumu mara kwa mara utawala kwa kupanga kupunguza ufadhili katika Idara ya Ustawi wa Jamii.