logo

NOW ON AIR

Listen in Live

Maelfu ya watu waandamana kumpinga Trump kote Marekani

Maelfu ya watu waliingia mitaani kote Marekani kupinga hatua zilizochukuliwa hivi majuzi na Rais Trump.

image
na BBC NEWS

Kimataifa20 April 2025 - 14:16

Muhtasari


  • Nje ya Ikulu ya White House na Tesla dealerships na katika vituo vya miji mingi, waandamanaji walitoa malalamiko mbalimbali. 
  • Maandamano ya kisiasa yanazidi kuwa ya kawaida nchini Marekani ambayo yamekuwa yakivutia makumi kwa maelfu.

Waandamaji Marekani

Maelfu ya watu waliingia mitaani kote Marekani siku ya Jumamosi kupinga hatua zilizochukuliwa hivi majuzi na Rais Donald Trump.

Kile kinachojulikana kama "50501", ikimaanisha "maandamano 50, majimbo 50, na kundi 1 la vuguvugu", maandamano hayo yalikusudiwa kwendana na kumbukumbu ya miaka 250 ya kuanza kwa Vita vya Mapinduzi vya Marekani.

Nje ya Ikulu ya White House na Tesla dealerships na katika vituo vya miji mingi, waandamanaji walitoa malalamiko mbalimbali. Wengi walitoa wito wa kurejeshwa kwa Kilmar Ábrego García, ambaye alifukuzwa kimakosa hadi El Salvador.

Maandamano ya kisiasa yanazidi kuwa ya kawaida nchini Marekani ambayo yamekuwa yakivutia makumi kwa maelfu katika miji nchini kote.

Umaarufu wa Trump unaonekana kudorora, haswa linapokuja suala la uchumi. Alipoingia madarakani Januari, kiwango chake cha kukubalika na watu kilikuwa 47%, kulingana na Gallup lakini katika kura ya hivi majuzi ya Reuters/Ipsos ilionyesha kuwa umaarufu wake umepungua hadi 43%.


RADIO JAMBO FREQUENCIES

Kisumu 100.1 | Mombasa 92.3 | Nakuru 96.9 | Eldoret 99.5 | Nyeri 99.3 | Nyahururu 97.3 | Webuye 95.3 | Meru 92.7 | Kitui 104.9 | Kibwezi 104.7 | Voi 105.7 | Malindi 98.1 | Lamu 104.7 | Narok 97.3 | Kapenguria 99.7 | Kisii 89.3 | Garissa 104.3 | Maralal 97.3 | Lodwar 92.7


logo© Radio Jambo 2024. All rights reserved