logo

NOW ON AIR

Listen in Live

[PICHA] China yaandaa gwaride kubwa kuadhimisha kumbukumbu ya miaka 80 ya ushindi wa Vita vya Pili vya Dunia

Rais Xi Jinping alisimamia gwaride na kukagua majeshi

image
na XINHUA

Kimataifa07 September 2025 - 21:30

Muhtasari


  • Majengo marefu yaliyoundwa kwa mfano wa Ukuta Mkubwa wa China yalisimama katika Uwanja wa Tian’anmen, yakibeba ishara ya ujasiri na mshikamano wa taifa la China katika kupinga uvamizi wa kigeni.
  • Rais Xi Jinping, ambaye pia ni Katibu Mkuu wa Kamati Kuu ya Chama cha Kikomunisti cha China na Mwenyekiti wa Tume Kuu ya Kijeshi, alisimamia gwaride na kukagua majeshi.

Kikosi cha kivita kisichotumia rubani cha angani kilihudhuria gwaride la kijeshi mjini Beijing, mji mkuu wa China, Septemba 3, 2025. China Jumatano iliandaa mkusanyiko mkubwa kuadhimisha kumbukumbu ya miaka 80 ya ushindi katika Vita vya Watu wa China vya Upinzani dhidi ya Uvamizi wa Kijapani na Vita vya Ulimwengu dhidi ya Ufashisti. (Xinhua/Xing Guangli)

China iliandaa gwaride kubwa la kijeshi katikati ya Beijing Jumatano kuadhimisha kumbukumbu ya miaka 80 ya ushindi wake katika Vita vya Pili vya Dunia, na kusisitiza dhamira ya nchi hiyo ya maendeleo ya amani katika dunia ambayo bado imejaa misukosuko na hali za kutokuwa na uhakika.

Kikosi cha kivita kisichotumia rubani cha majini kilihudhuria gwaride la kijeshi mjini Beijing, Septemba 3, 2025. (Xinhua/Xu Bingjie)


Wanajeshi walifyatua mizinga ya heshima wakati wa mkusanyiko mkubwa wa kumbukumbu hiyo mjini Beijing, Septemba 3, 2025. (Xinhua/Mu Yu)


Kikosi cha walinda amani wa China chini ya Umoja wa Mataifa kilihudhuria gwaride hilo. (Xinhua/Jiang Kehong)


Kikosi cha mashambulizi ya ardhini kilishiriki katika gwaride hilo. (Xinhua/Jiang)


Kikosi cha ulinzi wa anga kutoka meli kilipita katika Uwanja wa Tian’anmen wakati wa gwaride la kijeshi. (Xinhua/Yao Dawei)

Kikosi cha makombora ya kupambana na meli kilihudhuria gwaride. (Xinhua/Li He)

Vikosi vya silaha vizito vilishiriki katika gwaride hilo. (Xinhua/Wang Peng)

Kikosi cha makombora ya mwendo wa kasi wa sauti kilihudhuria gwaride. (Xinhua/Zhang Tao)

Kikosi cha ndege za mafuta na ndege zinazopokea mafuta hewani kilishiriki katika gwaride hilo. (Xinhua/Sun Fanyue)

Picha hii iliyopigwa Septemba 3, 2025 inaonesha kikosi cha ndege za kivita. (Xinhua/Bai Xueqi)

Makala Zinazohusiana


RADIO JAMBO FREQUENCIES

Kisumu 100.1 | Mombasa 92.3 | Nakuru 96.9 | Eldoret 99.5 | Nyeri 99.3 | Nyahururu 97.3 | Webuye 95.3 | Meru 92.7 | Kitui 104.9 | Kibwezi 104.7 | Voi 105.7 | Malindi 98.1 | Lamu 104.7 | Narok 97.3 | Kapenguria 99.7 | Kisii 89.3 | Garissa 104.3 | Maralal 97.3 | Lodwar 92.7


logo© Radio Jambo 2024. All rights reserved