Xi Jinping, Katibu Mkuu wa Kamati Kuu ya Chama cha Kikomunisti cha China na Rais wa China, akifanya mazungumzo na Kim Jong Un, Katibu Mkuu wa Chama cha Wafanyakazi wa Korea na Rais wa Masuala ya Serikali ya Jamhuri ya Kidemokrasia ya Watu wa Korea (DPRK), katika Nyumba ya Wageni ya Serikali ya Kumsusan mjini Pyongyang, DPRK, Juni 8, 2026. (Xinhua/Yan Yan)Rais wa China na Katibu Mkuu wa Kamati Kuu ya Chama cha Kikomunisti cha China, Xi Jinping, amesema Jumatatu kwamba China na Jamhuri ya Kidemokrasia ya Watu wa Korea (DPRK) zinapaswa kuimarisha msingi wa kuaminiana kisiasa na kuinua kiwango cha ushirikiano wa vitendo.
Xi alitoa kauli hiyo wakati wa mazungumzo yake na Kim Jong Un, Katibu Mkuu wa Chama cha Wafanyakazi wa Korea na Rais wa Masuala ya Serikali ya DPRK.
Xi alisema kuwa baada ya miaka saba, amefurahi kurejea tena katika jiji zuri la Pyongyang, na kwamba anahisi ukaribu na uchangamfu wa kipekee.
Alisema yuko tayari kushirikiana na Kim kutumia ziara hiyo kama fursa ya kuimarisha mipango ya ngazi ya juu na mwongozo wa kimkakati katika mahusiano ya China na DPRK katika enzi mpya, kuhakikisha uhusiano wa pande mbili unaendelea kwenda sambamba na nyakati na kupata maendeleo makubwa zaidi.
Xi alisisitiza kuwa China na DPRK ni mataifa ya kijamaa yanayoongozwa na vyama vya kikomunisti, na kwamba urafiki wa jadi kati ya nchi hizo mbili umejengwa juu ya imani na malengo ya pamoja, pamoja na msingi imara wa kihistoria, kisiasa na kihisia.
Alibainisha kuwa urafiki unaorithishwa kutoka kizazi hadi kizazi, mustakabali wa pamoja na kusaidiana kwa dhati vimekuwa alama kuu za mahusiano kati ya China na DPRK.
Xi alisema kuwa bila kujali mabadiliko ya hali ya kimataifa, msimamo wa China wa kuthamini urafiki wa jadi na DPRK hautabadilika. Aliongeza kuwa msaada wa China kwa Kim katika kuongoza maendeleo ya ujamaa nchini DPRK na dhamira ya kulinda maslahi ya pamoja ya nchi hizo mbili pia hautayumba.
Akizungumzia mabadiliko makubwa yanayoendelea duniani, Xi alisema pande zote mbili zinapaswa kuangalia mambo kwa mtazamo mpana na wa muda mrefu, kujifunza kutoka historia ya mahusiano yao na kutumia fursa zinazojitokeza ili kuupa urafiki wao nguvu mpya zinazolingana na mahitaji ya wakati wa sasa.
Katika mazungumzo hayo, Xi alipendekeza hatua nne za kuendeleza mahusiano ya China na DPRK.
Kwanza, alisema pande zote mbili zinapaswa kuendelea kuongozwa na mawasiliano ya viongozi wa ngazi ya juu ili kuimarisha zaidi kuaminiana kisiasa. Alisisitiza kuwa mwongozo wa viongozi wa nchi hizo mbili ndio nguvu kubwa zaidi ya mahusiano yao.
Xi alibainisha kuwa mwaka huu ni kumbukumbu ya miaka 65 tangu kutiwa saini kwa Mkataba wa Urafiki, Ushirikiano na Msaada wa Pamoja kati ya China na DPRK, na kwamba nchi hizo zitafanya maadhimisho makubwa ya tukio hilo.
Pili, alisema ushirikiano wa vitendo unapaswa kupewa kipaumbele kwa manufaa ya wananchi. China iko tayari kushirikiana na DPRK katika kuoanisha mikakati ya maendeleo na kupanua ushirikiano katika biashara, kilimo, ujenzi, sayansi na teknolojia pamoja na huduma za afya.
Xi pia alihimiza matumizi ya fursa inayotokana na kufunguliwa tena kwa mipaka na kurejeshwa kwa safari za ndege za kiraia na treni za abiria za kimataifa ili kuongeza mawasiliano kati ya wananchi wa nchi hizo mbili.
Tatu, alisisitiza umuhimu wa kuendeleza urafiki wa jadi kwa kuimarisha mahusiano ya watu kwa watu. Alisema urafiki wa China na DPRK uliyojengwa kupitia historia ya mapambano ya pamoja ni urithi muhimu wa mataifa hayo mawili.
China, alisema, iko tayari kushirikiana na DPRK kuhifadhi maeneo ya kumbukumbu ya mashujaa wa Jeshi la Kujitolea la Watu wa China waliopigana nchini DPRK, pamoja na kuendeleza programu za elimu ya vijana na historia ya mapinduzi.
Nne, Xi alitoa wito wa kuimarishwa kwa uratibu wa kimkakati kwa kuzingatia misingi ya haki na usawa. Alisema maono yake ya kujenga jumuiya yenye mustakabali wa pamoja kwa wanadamu pamoja na mipango minne ya kimataifa yamelenga kuifanya utawala wa dunia kuwa wa haki zaidi na yamepokelewa vyema na jumuiya ya kimataifa, ikiwemo DPRK.
Akisisitiza kuwa Asia ni makazi ya pamoja ya nchi za eneo hilo, Xi alisema China na DPRK zinapaswa kuimarisha uratibu wa kimkakati, kulinda kwa pamoja mamlaka yao ya kitaifa, usalama na maslahi ya maendeleo, na kuchangia amani na maendeleo ya kikanda.
Xi Jinping, Katibu Mkuu wa Kamati Kuu ya Chama cha Kikomunisti cha China na Rais wa China, akifanya mazungumzo na Kim Jong Un, Katibu Mkuu wa Chama cha Wafanyakazi wa Korea na Rais wa Masuala ya Serikali ya Jamhuri ya Kidemokrasia ya Watu wa Korea (DPRK), katika Nyumba ya Wageni ya Serikali ya Kumsusan mjini Pyongyang, DPRK, Juni 8, 2026. (Xinhua/Xie Huanchi)
DPRK, Juni 8, 2026. (Xinhua/Li Xiang)Xi Jinping, Katibu Mkuu wa Kamati Kuu ya Chama cha Kikomunisti cha China na Rais wa China, akifanya mazungumzo na Kim Jong Un, Katibu Mkuu wa Chama cha Wafanyakazi wa Korea na Rais wa Masuala ya Serikali ya Jamhuri ya Kidemokrasia ya Watu wa Korea (DPRK), katika Nyumba ya Wageni ya Serikali ya Kumsusan mjini Pyongyang
DPRK, Juni 8, 2026. (Xinhua/Yin Bogu)Pyongyang, Katibu Mkuu wa Chama cha Wafanyakazi wa Korea na Rais wa Masuala ya Serikali ya Jamhuri ya Kidemokrasia ya Watu wa Korea (DPRK), katika Nyumba ya Wageni ya Serikali ya Kumsusan mjini Kim Jong Un, Katibu Mkuu wa Kamati Kuu ya Chama cha Kikomunisti cha China na Rais wa China, akifanya mazungumzo na Xi Jinping
Xi Jinping, general secretary of the Communist Party of China Central Committee and Chinese president, holds talks with Kim Jong Un, general secretary of the Workers' Party of Korea and president of the State Affairs of the Democratic People's Republic of Korea (DPRK), at the Kumsusan State Guesthouse in Pyongyang, the DPRK, June 8, 2026. (Xinhua/Yin Bogu)





