logo

NOW ON AIR

Listen in Live

"Leo umepewa mzee!" Mandonga amshambulia Wanyonyi baada ya ushindi mwingine Kenya

Mandonga alisema Jumamosi Wanyonyi alipewa  mpinzani mzee na dhaifu na ndio maana alishinda.

image
na Radio Jambo

Habari26 March 2023 - 06:29

Muhtasari


•Mandonga ambaye anajulikana kwa ucheshi wake mwingi alishinda pambano hilo la kusisimua katika raundi ya nane.

•Alimtupia vijembe bondia wa Kenya Daniel Wanyonyi aliyepiga mwezi Januari huku akiapa kurejea na kumpiga tena.

Bondia wa Tanzania Karim Mandonga alipata ushindi wake wa pili nchini Kenya mwaka huu baada ya kumpiga bondia wa Uganda Kenneth Lukyamuzi usiku wa Jumamosi katika ukumbi wa Kasarani Gymnasium, Nairobi.

Mandonga ambaye anajulikana kwa ucheshi wake mwingi alishinda pambano hilo la kusisimua katika raundi ya nane.

"Huyu Lukyamuzi, pambano la leo  Mungu kamsaidia mpaka kafika raundi ya kumi, lakini alikuwa anapoteza maisha. Wakati wowote, muda wowote, Mandonga Mtu Kazi ni mtu wa kazi," Mandonga alisema baada ya ushindi huo.

Bondia huyo alitoa shukrani za dhati kwa Watanzania na Wakenya kwa sapoti kubwa ambayo wamekuwa wakimpatia.

"Namshukuru mwenyezi Mungu kwa Watanzania wote. Namshukuru Mwenyezi Mungu kwa watu wa Kenya wote. Rais wa Kenya Mungu ambariki. Rais wa Chama cha michezo cha Ndondi pia Mungu ambariki," alisema.

Aliendelea kumtupia vijembe bondia wa Kenya Daniel Wanyonyi aliyepiga mwezi Januari huku akiapa kurejea na kumpiga tena.

Bondia huyo mwenye mbwembwe nyingi alisema Wanyonyi alipewa  mpinzani mzee na dhaifu siku ya Jumamosi na ndio maana alishinda.

"Nashukuru leo Mandonga Mtu Kazi leo nimekuja Kenya na nikaonyesha juhudi zangu. Na hii salamu inaenda kwa Daniel Wanyonyi, leo umepewa mzee wewe. Mimi nina kazi na wewe. Nakuja tena Kenya, nakuja kukushughulikia wewe. Naskia maneno yako unachochi, kawaida mimi najua kuongea na kutenda," alisema.

Mwezi Januari, Mandonga alipambana na Daniel Wanyonyi na kumshinda katika raundi ya 5 kwa muondoano wa kitaalamu.

Bondia huyo alikuwa amelitangaza sana pambano hilo lililochezewa KICC akisema kuwa ngumi aliyokuwa amemwandalia Wanyonyi ilikuwa na asili kutoka kwa milipuko ya mabomu katika vita vya Urusi na Ukraine kwa jina Sugunyo.

Na kweli kwa maneno yake, aliweza kumchachawiza Wanyonyi na kuzidisha tantarira zake baada ya kushinda.

Ushindi huo wa kukumbukwa uliweza kumtuza kwa gari mbili ambazo alizawadiwa na wafadhili wawili tofauti.


RADIO JAMBO FREQUENCIES

Kisumu 100.1 | Mombasa 92.3 | Nakuru 96.9 | Eldoret 99.5 | Nyeri 99.3 | Nyahururu 97.3 | Webuye 95.3 | Meru 92.7 | Kitui 104.9 | Kibwezi 104.7 | Voi 105.7 | Malindi 98.1 | Lamu 104.7 | Narok 97.3 | Kapenguria 99.7 | Kisii 89.3 | Garissa 104.3 | Maralal 97.3 | Lodwar 92.7


logo© Radio Jambo 2024. All rights reserved