logo

NOW ON AIR

Listen in Live

'Alikuwa ananichapa' Saumu Mbuvi afunguka kuhusu Ben Gatu

'Alikuwa ananichapa' Saumu Mbuvi afunguka kuhusu Ben Gatu

image
na

Mahakama02 October 2020 - 03:05
Hii leo kwenye kitengo cha Ilikuaje, mwanawe gavana wa Nairobi, Saumu Mbuvi ndiye aliyekuwa mgeni wetu.

Akizungumza na Massawe Japanni, Saumu Mbuvi alifunguka wazi wazi vile ambavyo baba ya mtoto wake wa kike, wa miaka mitatu alikuwa anampiga walipokuwa na uhusiano.

Wapenzi hawa wa zamani walikata kauli kutia kikomo uhusiano wao baada ya miezi tisa kwani Ben Gatu alikuwa na tabia ya kumpiga.

Zaidi ya hayo, Saumu alisimulia kuwa Ben Gitau alimwacha amlee mtoto wao peke yake na ikabidi ajikaze kisabuni ili mtoto wake asikose lolote.

kadhalika, Saumu aliwapa mawaidha wanawake wote waliokosana na baba ya watoto wao, na kuwahimiza kuwa waweze kutafuta mpenzi mwengine kwani baba ni mtu muhimu sana kwa maisha ya mtoto.

Akisimulia vile ambavyo maisha ya uhusuiano wa kimapenzi na Ben Gatu yalikuwa, Saumu alisisitiza kuwa mapenzi yao hayakuwa matamu katu.

Baada ya kukatiza uhususiano wao, Saumu alibaki na huzuni tele kwani alipata uja uzito akiwa bado binti mdogo bado wa miaka ishirini na moja.

Saumu alipaswa kurudi kwa baba yake na kujinyenyekeza kwani maisha ya ndoa yalimshinda. Aisee! mwenda tezi na omo,marejeo ni ngamani.

Kwa sasa hivi, Seneta wa Lamu, bwana Anwari Loitiptip, ndiye mpenzi wake Saumu, na baba ya mtoto wake wa miaka tatu sasa. Kulingana na vile ambavyo alisimulia hadithi yake, tuna uhakika kuwa Bwana Anwari anampenda na kumtunza binti Saumu pamoja na mtoto wake.

Maarufu Zaidi

RADIO JAMBO FREQUENCIES

Kisumu 100.1 | Mombasa 92.3 | Nakuru 96.9 | Eldoret 99.5 | Nyeri 99.3 | Nyahururu 97.3 | Webuye 95.3 | Meru 92.7 | Kitui 104.9 | Kibwezi 104.7 | Voi 105.7 | Malindi 98.1 | Lamu 104.7 | Narok 97.3 | Kapenguria 99.7 | Kisii 89.3 | Garissa 104.3 | Maralal 97.3 | Lodwar 92.7


logo© Radio Jambo 2026. All rights reserved