Kurugenzi wa mashtaka ya umma (DPP) imeshinda kesi dhidi ya mwanamke aliyeshtakiwa kwa madai ya kuhusika katika ulanguzi wa dawa za kulevya katika jiji la Mombasa
Katika hukumu iliyosomwa na hakimu David Odhiambo kwa niaba ya hakimu Martin Rabera, mshukiwa alipatikana na hatia ya ulanguzi wa heroine ya kilo 91.738 mnamo Septemba 20, 2018 katika mtaa wa Kikambala kwenye kaunti ya Kilifi. Herione hiyo kwa mujibu wa ushahidi uliowalishwa mbele ya mahakama hiyo iligharimu shilingi milioni 275.214.
Upande wa mashtaka ukiongozwa na Barbara Sombo, ulieleza mahakama kuwa dawa hiyo ya kulevya ilikuwa imewekwa katika masanduku mawili ya rangi ya kahawia na mfuko mmoja mdogo ikiwa katika hifadhi kwenye nyumba moja.
Hakimu Rabera alisema kuwa upande wa mashtaka uliwasilisha ushahidi wa kutosha ikiwemo ushuhuda kutoka kwa maafisa ambao waliendesha msako katika makao ya mshukiwa.
Aidha kesi ilichukua mkondo tofauti wa kutupilia mbali mashtaka dhidi ya mume wa mshukiwa baada ya kuaga dunia. Mshukiwa alishtakiwa pamoja na mumewe aliyejulikana maarufu kama Kandereni ila aliaga siku tisa baada ya kuripotiwa kupotea kwa njia zisizoeleweka.
Akitoa hukumu hiyo, hakimu Rabera alisema kuwa hakukuwa na upungufu katika ushahidi uliowasilishwa mahakamani wa kudai kuwa dawa hizo za kulevywa zilipandikizwa nyumbani kwa mshukiwa.
“Hakuna mianya katika ushahidi wa kuonyesha kwamba dawa hizo zilihitilafiwa ama kuweka, baada ya kupitia na kuchambua ushahidi, Napata mashtaka dhidi ya mshukiwa kuwa ukweli bila ya shaka yoyote.” Alisema hakimu Rabera katika hukumu yake.
Aidha mshukiwa vile vile ametakiwa kulipa faini ya shilingui
milioni 600.