OCPD wa Kibwezi Ben Changulo anasema majambazi hao ambao walimjeruhi pia meneja wa kilabu hicho walifanikiwa kuiba shilingi elfu mbili pamoja na mali nyingine.
"Ilikuwa saa kumi na moja ambapo watu waliingia wakiwa wamejihami, wakamjeruhi maneja wa klabu hicho kisha kumuuwa bawabu," Alielezea Ben.
Uvamizi huo unajiri mwezi mmoja tu baada ya mfanyibiashara mwingine wa Mpesa mjini humo kuuliwa kwa kupigwa risasi na majambazi.
Shuguli za usafiri wa kawaida zilitatizika kwa muda kwenye barabara ya Mamboleo - Miwani, kaunti ya Kisumu baada ya wahudumu wa bodaboda eneo hilo kushiriki maandamano ili kulalamikia hali mbovu ya barabara sehemu hiyo.
"Hapa mamboleo tunaumia, vumbi inajaa kwa macho na madaktari wamegoma hawawezi kutuhudumia, tunauchungu kwa maana tunaenda katika hospitali ya kibinafsi ambayo ni mepa nyingi tunaomba Anyang'Nyong'o atusaidie," Alizungumza mwanabodaboda.
"Barabara imejaa vumbi takataka zina pita hapa na lori hawataki kujua sisi ni akina nani wanapita hapa mbio hata hatuwezi fanya kazi nio maana tumefunga barabara," Alisema mwendeshaji mmoja wa pikipiki.
