“At first he stopped me but I convinced him, and he paid my fees after I promised to finish my public health course,” Nyc alisema.
Nyc alikazana na kusoma kozi yake ya afya ya jamii na pia udj na baada ya miaka minne, alihitimu na kozi hiyo ya afya ya jamii. Hata hivyo, alisema na kusisitiza kuwa, hajawahi tumia digrii ile na mpaka wakati huu, mama yake humwona kama binti asiye na kazi.
“I have never used the degree anywhere and my mum still thinks I’m jobless.”
Safari ya udj, haijakuwa rahisi, kwani dj wengi wa kiume huwaona dj wa kike kuwa tishio kwao na kwa hivyo, wanakutishia na wengine kutaka kushirikiana na wewe kimapenzi ili wakupe kazi.
“There is discrimination in the industry as some male DJs see you as a threat and try to fight you while others want to [sleep with you] to give you gigs,” alisema.
Zaidi ya hayo, Nyc alisema kuwa, ni vigumu sana kupata mpenzi kwani, wanaume wengi huogopa kumchumbia binti anayefanya kazi usiku kwani kazi yao huwabidi waende wafanye kazi usiku.
Vilevile, Nyc alisema kuwa kufanya kazi na Mbusi na Lion ni kitu bora sana kwani watu hawa, wamemsaidia vilvyo .
“They are the best duo to work with and through them, I am now known and they have been helping me get gigs,” Nyc alisema.
Mwisho, ujumbe wake kwa mabinti wanaotaka kuwa Dj ni kuwa wajue kwamba mambo hayatakuwa rahisi wanapoanza kazi hii lakini kuangazia, na kuzingatia yale ambayo unataka kupata maishani ndio ufunguo wa kufaulu kama dj wa kike.
"It won’t be easy at the start, but focusing on what you want to achieve is the key.”Dj Nice alisema.