logo

NOW ON AIR

Listen in Live

Mwanablogu Cyprian Nyakundi afikishwa kortini .

Mwanablogu Cyprian Nyakundi afikishwa kortini .

image
na

Burudani02 October 2020 - 04:47
  Mwanablogu Cyprian Nyakundi  ameshtakiwa kwa njama ya  ulaghai wa shilingi milioni 17.5 .Amefikishwa mbele ya hakimu  mkuu  wa Milimani  na kukanusha mashtaka dhidi yake .

Stakabadhi ya mashtaka imesema  kwamba mnamo januari tarehe 20 mwezi huu katika  jumba la westgate Mall  Nyakundi na wengine ambao hawaku kortini walimpunja shilingi milioni 1 Yogesh Pattni ambaye ni afisa mkuu mtendaji wa Benki ya  Victoria Commercial Bank Ltd,  kama sehemu ya malipo ya shilingi milioni 17.5 ili kuondoa chapisho waliloweka mtandaoni . Kesi ya upande wa mashtaka ni kwamna Nyakundi aliitisha pesa  kama shari la kuondoa chapisho hilo  ambalo lilikuwa linaichafulia jina benki hiyo  na wafanyikazi .

Wakili wa mlalamishi  Kamau Chege amesema  Nyakundi  anakaidi agizo la mahakama kwani amekuwa akiendelea kuweka mtandaoni  taarifa   za kuwachafulia jina watu na taasisi mbali mbali . Nyakundi na Mtuhumiwa mwenzake Emmanuel Nyamweya Ongera  wameachiliwa kwa bondi ya shilingi milioni kila mmoja   au dhamana mbadala ya shilingi laki tatu pesa taslimu kila mmoja .Kesi hiyo itatajwa Fberuari tarehe 7 .

Maarufu Zaidi

RADIO JAMBO FREQUENCIES

Kisumu 100.1 | Mombasa 92.3 | Nakuru 96.9 | Eldoret 99.5 | Nyeri 99.3 | Nyahururu 97.3 | Webuye 95.3 | Meru 92.7 | Kitui 104.9 | Kibwezi 104.7 | Voi 105.7 | Malindi 98.1 | Lamu 104.7 | Narok 97.3 | Kapenguria 99.7 | Kisii 89.3 | Garissa 104.3 | Maralal 97.3 | Lodwar 92.7


logo© Radio Jambo 2026. All rights reserved