logo

NOW ON AIR

Listen in Live

'Nina imani Harambee Stars italaza Comoros,' Ghost Mulee

Kocha  mkuu wa Harambee stars Jacob “Ghost” Mulee anai imani Kenya itawalaza Comoros katika mechi ya kufuzu AFCON Jumatatno ijayo, baada ya wachezaji wake kuonyesha udhabiti mkubwa kambini. Ghost anawaongoza wachezaji  ugani Kasarani, huku Ayub Timbe, Teddy Akumu na Cliff Nyakeya wakiwa wachezaji  wa peke wa kulipwa  waliofika kambini.

image
na Radio Jambo

Dakia-udaku07 November 2020 - 06:27
kocha ghost mulee

Kocha  mkuu wa Harambee stars Jacob “Ghost” Mulee anai imani Kenya itawalaza Comoros katika mechi ya kufuzu AFCON Jumatatno ijayo, baada ya wachezaji wake kuonyesha udhabiti mkubwa kambini. Ghost anawaongoza wachezaji  ugani Kasarani, huku Ayub Timbe, Teddy Akumu na Cliff Nyakeya wakiwa wachezaji  wa peke wa kulipwa  waliofika kambini.

Wachezaji wengine akiwemo nahodha Victor Wanyma wanatarajiwa wikendi hii. 

Mlinzi wa kimataifa wa Kenya David  Cheche Ochieng amejiunga na Mathare United kwa mkataba wa mwaka mmoja.

Cheche  anayeondoka Al Ansar  ya Saudi Arabia, hapo awali alichezea Tusker na  AFC Leopards  na alishinda kombe la ligi kuu na wanamvinyo. Cheche anatarajiwa kuleta uzoefu mkubwa baada ya wachezaji mashuhuri  kuhama  klabu hio msimu huu.

Comoros imetangaza kuwa mashabiki wataruhusiwa kutazama moja kwa moja mechi yao na Harambee stars nchini humo. Licha ya janga la corona kukita mizizi, maafisa wa kisiwa hicho wameamua mashabiki elfu 5,  pekee watakubaliwa uwanjani.

Kenya itaalika Coromos katika mkondo wa kwanza wa kufuzu kwa AFCON  Jumatano ijayo ugani Nyayo bila mashabiki, kabla ya mechi ya marudiano  wikendi ijayo.

Kwingineko, wasmamizi wa ligi ya daraja la  pili nchini  Uingereza, wamethibitisha kuwa  klabu ya  Derby County imenunuliwa na  bwenyenye wa  Abu Dhabi Sheikh Khaled. Kabla ya kununua hisa kubwa zaidi katika klabu hiyo ya EFL  Khaled hapo awali alijaribu kununua  Liverpool na  Newcastle United ila hawakufanikiwa.

Hii ina maana kuwa atawekeza katika klabu hiyo na  angalau kuwapandisha katika ligi kuu Uingereza.    

 


RADIO JAMBO FREQUENCIES

Kisumu 100.1 | Mombasa 92.3 | Nakuru 96.9 | Eldoret 99.5 | Nyeri 99.3 | Nyahururu 97.3 | Webuye 95.3 | Meru 92.7 | Kitui 104.9 | Kibwezi 104.7 | Voi 105.7 | Malindi 98.1 | Lamu 104.7 | Narok 97.3 | Kapenguria 99.7 | Kisii 89.3 | Garissa 104.3 | Maralal 97.3 | Lodwar 92.7


logo© Radio Jambo 2024. All rights reserved