Gavana wa kaunti ya Makueni Kivutha Kibwana ametangaza kuwa atawania kiti cha urais wakati wa uchaguzi mkuu wa mwaka wa 2022.
Kupitia kwenye ukurasa wake wa facbook kibwana alikuwa na haya ya kusema,
"Naomba nihudumu kama rais wenu kuanzia 2022. Natafuta uungwaji mkono na Kongamano La Mageuzi ( KLM)
"KLM ni muungano wa mashirika ya kutetea haki na wanaoleta mageuzi kwenye vyama vya kisiasa. Tutaunda muungano wa kuleta ushindi." Aliandika KIbwana.
Kivutha ameungana na kiongozi wa Narc Kenya Martha Karua, mwanaharakati David Ndii, Bonface Mwangi na wengine chini ya vuguvugu la Linda Katiba.
Aliingia kwenye siasa 2002 wakati ambapo alichaguliwa kama mbunge wa Makueni na kisha kuzawadiwa na aliyekuwa rais Mwai Kibaki na kiti cha uwaziri.
