Mahusiano kati ya watu yana vituko na wakati mwingine ,una visa vya kushangaza na vingine vya kutisha . wamesumulia wanawake kadhaa kuhusu mateso waliyopitia mikononi mwa wanaume ambao waliwaadhibu kwa njia kadhaa ambazo ziliwatia mashakani .Hebu soma kuhusu jinsi wanaume walivyotoa adhabu kwa njia mbali kwa wanawake hawa ;
Utachonga viazi
Annete hakujua kwamba hatua yake ya kutaka kuachana na mpenzi wake wa wakati huo ingemfanya kujipata katika jikoni ya hoteli walimokuwa akichonga viazi na kusafisha vyombo. Lakini mambo yalianza vizuri na wakati John aliposema yuataka kumuona ili wasuluhishe tofauti kato yao hakujua hasira zake zitamfikisha kiwango kipi aiposimama kidete na msimamo wake kwamba hawawezi kurudiana .Katika hoteli waliokwenda , mtoto wa kike alikuwa ameitisha kuku ,wali na glasi nzito ya jusi . Alijua kama kawaida baada ya amzungumzo yao ni John ndiye angelipa bili lakini kwa sababu mazungumzo hayakwenda alivyotaka ,John aliondoka akisema anaingia msalani na hivyo ndivyo alivyomuacha Annete na mzigo wa bili ya chakula chake na cha John na pia hakuwa na nauli kwani hakubeba hata shilingi . Hiyo ndio adhabu ambayo hadi sasa Annete hajaisahau na wakati wote amekuwa anajihami kwa pesa zake akienda date na mwanamme yeyote .
Kuacha nje ya gari usiku
Baada ya siku wa burudani na vileo Susan alikuwa amechoka na hawezi kujielekewa .usiku katika mkahawa wa carnivore ulikuwa mrefu na burudani haikuwa chache .wakati walipokuwa wakiondoka kuelekea nyumbani mwendo wa saa kumi na moja alfajiri akiwa pamoja na mpenzi wake Benson ,walitofautiana iwapo Benson angeelekea kazini moja kwa moja na kumchukulia teksi Susan au amfikishe nyumani ndiposa arudi kazini . Susan hakutaka kushuka kutoka garini kwa sababu ya kibaridi hicho cha asubuhi lakini kwa hasira ,Mpenzi wake alisimamisha gari na kumlazimisha kutoka nje –alimuacha hapo na huo ndio uliokuwa mwisho wa uhusiano wao .
Simu kwa maji
Wakati wote Elisa akizungumza na mpenzi wake Edwin ,alikuwa tu kwenye simu yake ya mkoni ,mara katumiwa ujumbe ,anaweza video akichekeshwa –mambo ambayo mwenzake hakupendezwa nayo . wakati mwingi alikuwa akimuonya kuhusu kuiweka simu kando ili wawe na muda wao lakini Elisa hakusikia . Siku moja alipoweka simu yake mezani ,kwa maksudi Edwin aliichukua na kuitumbukiza katika jagi ilyokuwa na maji ,kisha akaitoa na kuiweka ilipokuwa bila Elisa kujua . Alipojaribu kuitumia simu yake ,ilikuwa imezima na haikuwaka .Elisa alipogundua kilichofanyika ,hasira zake hazikumruhusu kuzungumza tena na Edwin ambaye alifanya hivyo ili kumpa somo mpenzi wake
Je,mpenzi wako wa zamani aliwahi kukufanyia nini kama njia ya kukuadhiabu?