Kenya imerekodi visa 1,463 vipya vya maambukizi ya COVID-19 kutoka kwa sampuli 8,976 katika muda wa saa 24 zilizopita.
Kufikia sasa Kenya imesajili jumla ya visa 126,170 kutoka kwa sampuli 1,443,701
Katika visa hivi vipya, 1428 ni raia wa Kenya huku 35 wakiwa raia wa kigeni, 802 ni wa kiume na 661 ni wanawake.
Mgonjwa mwenye umri wa chini ana miezi tatu huku mwenye umri wa juu akiwa na miaka 103.
Kulingana na takwimu za wizara ya afya watu 498 wamepona virusi vya corona, 372walipona wakiwa nyumbani huku 126 wakipona wakiwa katika hospitali mbali mbali, na kufikisha idadi jumla ya 91,268 ya watu waliopona.
Hata hivyo habari za kuhuzunisha ni kwamba watu 26 waliaga dunia kutokana na maambukizi kufikisha 2,096watu waliofariki kutokana na maambukizi ya virusi vya corona.
Jumla ya wagonjwa 1,080 wamelazwa katika vituo mbali mbali vya afya , huku 3,825wakiuguzwa nyumbani.
Wagonjwa 121 wamo katika kitengo cha wagonjwa mahututi (ICU)
