Msanii tajika wa nyimbo aina ya Bongoflava, Diamond Platnumz ameisuta kampuni ya Forbes kwa kumuweka kwenye orodha ya wanamuziki tajiri zaidi Afrika.
Mwanamuziki huyo tokea Tanzania amewasihi Forbes kufanya utafiti dhabiti kabla ya kuweka jina lake kwenye orodha ya wanamuziki tajiri zaidi Afrika.
“Wakatimwingine mfanye utafiti mzuri ili mdhibitishe thamani yangu ya kweli kabla ya kuweka jina langu kwenye orodha yenu ya kishenzi ya wanamuziki tajiri zaidi Afrika” Diamond aliandika kwenye ukurasa wake wa Instagram.
Kulingana na orodha iliyotolewa na shirika la Forbes hivi majuzi, Diamond hayupo miongoni mwa wanamuziki tajiri zaidi Afrika wa kwanza ishirini.