logo

NOW ON AIR

Listen in Live

"Pesa anazonilipa zanitosha kulala tu" Mkubwa Fella afichua mshahara anaolipwa na Diamond kumsimamia

Fella alisema kuwa pesa anazomlipa Diamond zinamtosha yeye kulala tu na kufurahia maisha bila kujihusisha na kazi zingine.

image
na Radio Jambo

Makala01 August 2021 - 11:54

Muhtasari


•Fella alifichua kuwa kila mwezi Diamond humlipa kiasi cha milioni 46 za Tanzania kusimamia shughuli za usanii wake.

•Meneja huyo pia alitaja kuwa huwa anapokea kiasi fulani cha pesa kutoka kwa nyota wengine anaosimamia kama Rayvanny, Zuchu na Mbosso.

Diamond Platnumz na Mkubwa Fella

Mkubwa Fella ambaye ni meneja wa staa wa Bongo Diamond Platnumz ameweka wazi mshahara ambao msanii huyo humlipa kila mwezi.

Alipokuwa anazungumza kwenye stesheni ya Wasafi nchini Tanzania, Fella alifichua kuwa kila mwezi Diamond humlipa kiasi cha milioni 46 za Tanzania kusimamia shughuli za usanii wake..

Fella alisema kuwa pesa anazomlipa Diamond zinamtosha yeye kulala tu na kufurahia maisha bila kujihusisha na kazi zingine.

"Hela ambayo nalipwa na Naseeb (Diamond) nina Haki ya kulala tu. Ijapokuwa kusema mshahara ni dhambi lakini mimi nachukua dola 20,000 kwa mwezi.. ni sawa na 45M kila mwezi"  Alisema Fella.

Mshahara wake Fella kutoka kwa Diamond kila mwezi ni zaidi ya milioni mbili za Kenya

Meneja huyo pia alitaja kuwa huwa anapokea kiasi fulani cha pesa kutoka kwa nyota wengine anaosimamia kama Rayvanny, Zuchu na Mbosso.

"Na bado nakwambia bado gawio kutoka kwa Rayvanny,bado gawio kutoka kwa Zuchu, bado gawio kutoka kwa Mbosso kwa sababu Mbosso ndio kinyago nimechonga mwenyewe." Fella alisema.

Fella alikiri kuwa muziki kweli walipa.


RADIO JAMBO FREQUENCIES

Kisumu 100.1 | Mombasa 92.3 | Nakuru 96.9 | Eldoret 99.5 | Nyeri 99.3 | Nyahururu 97.3 | Webuye 95.3 | Meru 92.7 | Kitui 104.9 | Kibwezi 104.7 | Voi 105.7 | Malindi 98.1 | Lamu 104.7 | Narok 97.3 | Kapenguria 99.7 | Kisii 89.3 | Garissa 104.3 | Maralal 97.3 | Lodwar 92.7


logo© Radio Jambo 2024. All rights reserved