logo

NOW ON AIR

Listen in Live

'Mungu saidia BBI tafadhali,'Babu Owino aomba huku mahakama ya rufaa ikusubiriwa kutoa uamuzi

Babu Owino aliandika ujumbe huku akimuomba Mungu asaidia BBI.

image
na Radio Jambo

Makala20 August 2021 - 12:01

Muhtasari


  • Babu Owino aomba huku mahakama ya rufaa ikusubiriwa kutoa uamuzi wa BBI
Babu Owino

Huku macho yote yakiwa kwenye mahakama ya rufaa, ili kutoa uamuzi wa BBI, baadhi ya wandani wa kinara wa ODM Raila Odinga wameanza kumuomba Mungu asaidia mchakato wa BBI.

Mapema wiki hii kinara huyo akiwa kwenye mahojiano alisema kwamba, mahakama ya rufaa ikitupilia mbali mchakato wa BBI, hawataharibu muda wa kuenda kwenye mahakama kuu.

Jopo la majaji saba wa mahakama ya rufaa wakiongozwa na Jaji Daniel Musinga wanatarajiwa kutoa uamuzi ambao utakuwa na athari kubwa kwa mchakato wa marekebisho ya katiba.

Rufaa hiyo iliwasilishwa na miongoni mwao rais Uhuru Kenyatta na kinara wa ODM Raila Odinga waliopinga uamuzi wa mahakama kuu uliyoharamisha mchakato wa marekebisho ya katiba maarufu BBI.

Kupitia kwenye ukurasa wake mbunge wa Embakasi Mashariki, Babu Owino aliandika ujumbe huku akimuomba Mungu asaidia BBI.

"Mungu saidia BBI tafadhali," Babu Owino aliandika.

Hizi hapa jumbe za wanamitandao baada ya ujumbe wake Owino;

Ali Dayib: We're also praying to God so that BBI dies a natural death.

Omondi Brian: This thing is coming down very fast than a super sonic jet, today we must celebrate the end of impunity.

Robert Kimutai: Today you are very humble!!!

Ben O. Osuga: God has heard you. Reggae will continue.. Inshallah!

Vitalis Kipkosgei:Babu as you are singing,no body can stop raggae..we husters sing.nothing but prayers

Huku jaji Tuiyott aitoa uamuzi wake kuhusu BBI alipuuzilia mbali rufaa ya IEBC,pia jaji Sichale alisema kwamba IEBC haikukosea kuhakiki saini zilizokusanywa kwa ajili ya BBI.

 

Maarufu Zaidi

RADIO JAMBO FREQUENCIES

Kisumu 100.1 | Mombasa 92.3 | Nakuru 96.9 | Eldoret 99.5 | Nyeri 99.3 | Nyahururu 97.3 | Webuye 95.3 | Meru 92.7 | Kitui 104.9 | Kibwezi 104.7 | Voi 105.7 | Malindi 98.1 | Lamu 104.7 | Narok 97.3 | Kapenguria 99.7 | Kisii 89.3 | Garissa 104.3 | Maralal 97.3 | Lodwar 92.7


logo© Radio Jambo 2026. All rights reserved