logo

NOW ON AIR

Listen in Live

Wasanii, mashabiki wajumuika kumtakia King Kaka afueni ya haraka baada ya kuwa akiugua kwa miezi mitatu

Kaka ameshauri watu kutosahau kuombea afya njema huku akisema kuwa paa za hospitali aghalabu huwa zinachosha.

image
na Radio Jambo

Habari11 September 2021 - 12:37

Muhtasari


•Kaka ameshauri watu kutosahau kuombea afya njema huku akisema kuwa paa za hospitali aghalabu huwa zinachosha.

Mwanamuziki tajika nchini Kennedy Ombima almaarufu kama King Kaka amekuwa akiugua kwa kipindi cha zaidi ya miezi mitatu iliyopita.

Mwanzoni mwa mwezi huu King Kaka alifichua kuwa hajakuwa na hisia ya ladha kwa kipindi cha miezi miwili na amekuwa akila matunda na kunywa uji tu.

Msanii huyo anayefahamika sana kwa kibao chake 'Wajinga nyinyi' alisema kuwa tangu aanze kuugua amepoteza kilo 33 na kiuno chake kimepungua na inchi tatu.

Mashabiki wangu, nimeona ni heri niwaambie haya. Nimekuwa mgonjwa kwa miezi mitatu na siku nane. Nilipimwa vibaya. Nimepoteza kilo 33 kwa wakati huo na tulianza kutembea hospitalini. Nimefanyiwa vipimo vyote na hakuna matokeo. Cha kushangaza ni kuwa sina maumivu yoyote na tunatumai kuwa tutapata suluhu hivi karibuni. Kiuno changu kilikuwa na ukubwa wa 36 na sasa ni 33" King Kaka aliandika kwenye ukurasa wake wa Instagram.

Kaka alisema kuwa hata nguo alizokuwa anavaa hapo awali hazimtoshei kwa sasa kufuatia kupungua kwa ukubwa wa kiuno chake.

Hata hivyo alieleza kuwa ana matumaini ya kupata nafuu hivi karibuni kuona kuwa alianza kula chakula takriban wiki tatu zilizopita

"Nilikuwa nanywa uji na kula matunda kidogo. Nilianza kula chakula wiki tatu zilizopita na polepole nitazoea. Sijakuwa na hisia ya ladha kwa miezi miwili" Alisema Kaka.

Siku ya Jumamosi Kaka alipakia picha akiwa amekalia kiti huku akiwa ameshika simu yake mkononi.

Kwenye picha hiyo mwanamuziki huyo alioneka kuwa mdhaifu huku akiwa amefunga bandeji kwenye mkono wake wa kulia.

Kaka ameshauri watu kutosahau kuombea afya njema huku akisema kuwa paa za hospitali aghalabu huwa zinachosha.

"Paa za hospitali huwa zinachosha sana. Kumbuka kuombea afya njema kila mara. Kwa sasa naangalia uwezekano wa Ronaldo kufunga mabao matatu leo dhidi ya Newcastle" Aliandika King Kaka chini ya picha hiyo.

Wanamitandao wengi ikiwemo wasanii na watu mashuhuri walijumuika chini ya chapisho la Kaka kumtakia afueni ya haraka.

@sleepydavid Bounce Back Time

@willy.paul.msafi All will be well my brother. Siunajua kuna God? Yes anakucheki.. utakua sawa bro much love fam

@daddiemarto Brooooo!! Welele! It shall be well

@michelle.ntalami Your healing journey begins

@wyredalovechild Get well soon King

@h_arttheband Quick recovery to you champ

@ogadaolunga Quick recovery bro

@loulou_hassan Utakuwa sawa Kaka Inshallah QR

Tazama jumbe zingine hapa:-

Kutoka Radio Jambo tunamtakia King Kaka kupona kwa haraka.


RADIO JAMBO FREQUENCIES

Kisumu 100.1 | Mombasa 92.3 | Nakuru 96.9 | Eldoret 99.5 | Nyeri 99.3 | Nyahururu 97.3 | Webuye 95.3 | Meru 92.7 | Kitui 104.9 | Kibwezi 104.7 | Voi 105.7 | Malindi 98.1 | Lamu 104.7 | Narok 97.3 | Kapenguria 99.7 | Kisii 89.3 | Garissa 104.3 | Maralal 97.3 | Lodwar 92.7


logo© Radio Jambo 2024. All rights reserved