Mwanaume mmoja mwenye umri wa miaka 41 amelazwa katika hospitali moja kaunti ya Murang'a akiwa hali mahututi baada ya kulawitiwa na genge la jamaa wanne
Mhasiriwa alikuwa anatembea kuelekea nyumbani kwake katika kijiji cha Githiagara, kaunti ndogo ya Kigumo mwendo wa saa saba usiku wa kuamkia Jumanne wakati masaibu yale yalimpata. Alikuwa ametoka kukata maji na wazee wengine.
Akiwa anayumbayumba kuelekea nyumbani, wanaume wanne wenye umri wa ujana walimjia na kumkokota hadi eneo lililojificha.
Pale walimuangusha chini na kumfanyia unyama ule wenye aibu kubwa mmoja baada ya mwingine na kumuacha akiwa hali mahututi.
Kufuatia hayo jamaa wawili, Bernard Kamande (25) na Erick Kimani (21) walikamatwa baada ya mhasiriwa kuwatambua.
Wawili hao wanazuiliwa katika kituo cha polisi cha Muthithi huku msako wa wenzao wawili ukiendelea.