Mwigizaji na mpenzi wa Akuku Danger, Sandra Dacha amesimulia maisha aliyokumbana nayo wakati alipokuwa akiibukia kwenye tasnia ya uigizaji.
Kupitia ukurusa wake wa instagram, Sandra alieleza kwamba alikuwa anaishi kwenye vitongoji duni Korogocho ambapo alikuwa analipa kodi ya nyumba shillingi 100.
Mwigizaji huyo wa Auntie Boss mwenye ubunifu na ustadi wa hali ya juu kuigiza alisema alielewa maisha ni hatua na yote hayo haliyapitia yanabaki kama kumbukizi kwake na mafunzo kwa wengine
Akisimulia a maisha yake alisema mapambano yake na maendeleo ya polepole yalifanya kuwa na imani kuwa kila kitu kinawezekana.
“Mwaka wa 2010 katika vitongoji duni vya Korogocho, hapa nilikuwa nimepanda daraja kutoka nyumba ya matope ambayo nilikuwa nalipa shilingi 100 tu, nilingia nyumba ya simiti ambayo nilikuwa nalipa shilingi 500, Nilikuwa nafurahia sana,”Sandra aliandika.