logo

NOW ON AIR

Listen in Live

Igathe adai kuidhinishwa na Tim Wanyonyi kuwa gavana wa Nairobi

•"Ninafuraha sana kuwaambia kuwa tayari wamenithibitishia kuwa wataniunga mkono kama gavana wa Kaunti ya Nairobi na tunaenda pamoja kama timu," Igathe alisema.

image
na Radio Jambo

Makala22 April 2022 - 03:41

Muhtasari


•"Ninafuraha sana kuwaambia kuwa tayari wamenithibitishia kuwa wataniunga mkono kama gavana wa Kaunti ya Nairobi na tunaenda pamoja kama timu," Igathe alisema.

Aliyekuwa naibu gavana wa Nairobi Polycarp Igathe Picha: MAKTABA

Mgombea kiti cha ugavana wa Nairobi Polycarp Igathe amefichua kuwa wagombeaji wengine wanaowania kiti hicho chini ya Azimio La Umoja Movement Coalition Party wamemwidhinisha.

Katika mahojiano yake na wanahabari Alhamisi jioni baada ya mkutano na Rais Uhuru Kenyatta katika Ikulu ya Nairobi, Igathe alisema kuwa sasa atapeperusha bendera ya Azimio.

"Ninafuraha sana kuwaambia kuwa tayari wamenithibitishia kuwa wataniunga mkono kama gavana wa Kaunti ya Nairobi na tunaenda pamoja kama timu," Igathe alisema.

Mkutano huo ulihudhuriwa na viongozi wengine wa Azimio, akiwemo kinara wa ODM Raila Odinga, Kalonzo Musyoka, Martha Karua miongoni mwa wengine.

Alisema kulikuwa na makubaliano kutoka kwa mkutano huo.

Hata hivyo, Igathe alisema kuwa uthibitisho huo ni wa mdomo, na kwamba uongozi wa Azimio unatarajiwa kutangaza suala hilo leo siku ya Ijumaa.

“Katika suala la mashauriano mazungumzo ya mdomo hayathibitishwi, kinachothibitishwa ni kile kinachotoka kwa viongozi wa chama chetu lakini kwa upande wangu nataka kuwapongeza.

Aliongeza kuwa hatua ya wawaniaji wengine kuacha azma zao ili kumuunga mkono ni kuhusu ushindi wa Azimio la umoja , na si kama watu binafsi.

Igathe alieleza imani yake kwamba Azimio itatoa tangazo hilo Ijumaa, ikiwa ni pamoja na jinsi nafasi nyingine zitakavyojazwa.

Haya yanajiri huku mwaniaji wa kiti cha ugavana wa Nairobi Tim Wanyonyi akisisitiza kuwa atawania ugavana Agosti 9.


RADIO JAMBO FREQUENCIES

Kisumu 100.1 | Mombasa 92.3 | Nakuru 96.9 | Eldoret 99.5 | Nyeri 99.3 | Nyahururu 97.3 | Webuye 95.3 | Meru 92.7 | Kitui 104.9 | Kibwezi 104.7 | Voi 105.7 | Malindi 98.1 | Lamu 104.7 | Narok 97.3 | Kapenguria 99.7 | Kisii 89.3 | Garissa 104.3 | Maralal 97.3 | Lodwar 92.7


logo© Radio Jambo 2024. All rights reserved