Wapiga kura wa Gereza sasa wanamtaka rais mpya atakayechaguliwa kuwasamehe kupitia uwezo wa rais wa huruma kuwasamea wafungwa.
Wafungwa katika Gereza kuu la Nakuru pia walishiriki katika zoezi hilo la kitaifa.
Wakizungumza baada ya kupiga kura siku ya Jumanne, wafungwa hao walisema msamaha wa rais wakati mwingine hupuuzwa na wale wanaopaswa kuufanyia kazi, wakitoa wito kwa rais mpya kurahisisha mchakato huo.
“Tunatumikia vifungo vya muda mrefu hapa na tunaamini kuwa atakayeshinda urais atatukumbuka. Hapo zamani, huruma ya rais ilipuuzwa na tunatarajia kwamba wengi watasamehewa miaka ijayo," Wafungwa hao walisema wakiongea na moja ya vyombo vya habari hapa nchini.
Mwangalizi kutoka Ofisi ya Msajili wa vyama vya siasa, David Mwaura, alisema zoezi la upigaji kura katika kituo hicho lilikuwa la amani na utulivu.
"Tumeshuhudia uchaguzi wa amani na ulioendeshwa vyema na IEBC lakini ningependa kusisitiza kuhusu mafunzo ya Maajenti. Maajenti wengi hawajui kile kinachohitajika kwao," Mwaura alisema.
Kwingineko ni kwamba kulikuwa na mkanganyiko katika Gereza la Kati la Kibos (B) huko Kisumu ambapo upigaji kura kwa wafungwa ulichelewa sana.
Afisa msimamizi Evans Owili alisema wana wapiga kura 15 waliojiandikisha katika kituo cha kupigia kura lakini kuchelewa kwa hiyo zoezi si kwa mnajili KIEMs wala sajili ya mwongozo.
