Leo ni krismasi kwa mataifa kadhaa duniani, yakiadhimisha kuzaliwa kwa Yesu Kristo. Wakristo wa dhehebu la Orthodox husheherekea Krismasi Januari 7, badala ya Disemba 25, iliyozoeleka na wengi. Unaweza kuiita Krismasi ya Orthodox.
Ni sikukuu inayopewa heshima kubwa kwa baadhi ya mataifa hasa ya magharibi. Rais wa Urusi, Vladmir Putin ametangaza mpaka kusitisha vita kwa saa 36 ili kuruhusu wananchi wa dhehebu hilo kusheherekea sikuu hiyo.
Nchini Ukraine leo ni mapumziko kama ilivyokuwa Disemba 25, 2022. Moja ya nchi zenye sherehe mbili za krismasi na zote zinatambulika na zimepewa hadhi sawa ya mapumziko ya sikukuu.
Krismasi ya Orthodox Ikoje?
Wakristo wa dhehebu la Orthodox hufuata kalenda tofauti na kalenda ya Gregorian ambayo kawaida hutumika katika nchi za Magharibi.
Wanasherehekea Krismasi tarehe 7 Januari, na sherehe zikianza rasmi usiku wa manane katika mkesha wao wa Krismasi.
Julius Caesar alianzisha kalenda katika 46BC kulingana na ushauri wa mwana-astronomia wa Misri Sosigene, ambaye alikuwa amehesabu mwaka wa mwezi.
Lakini vipimo vyake havikuwa sahihi kwa takriban dakika 11, na kwa karne nyingi tarehe za sikukuu kuu za Kikristo zilikuwa zimebadilika sana na ikawa hoja ya mjadala.
Ili kurekebisha hili, kalenda ya Gregorian ilianzishwa na Papa Gregory mwaka wa 1582, na hii ndiyo ambayo mataifa ya Magharibi na na maeneo mengi duniani bado yanaitumia leo.
Hispania, Ureno, Ufaransa, Poland, Italia na Luxemburg yalikuwa mataifa ya mwanzo mwanzo kuipitisha.
Nchi zinazosheherekea Krismasi Januari 7
Ukiacha mataifa yaliyotajwa hapo juu, mataifa mengine duniani yanayoshehereklea Krisimasi Januari 7 ni pamoja na;
- Bulgaria
- Belarus
- Egypt
- Ethiopia
- Eritrea
- Georgia
- Israel
- Kazakhstan
- Macedonia
- Moldova
- Montenegro
- Serbia