logo

NOW ON AIR

Listen in Live

Msanii Justin Bieber akatiza safari zake za 'Justice tour dates'

Justin Bieber alighairi ziara zake ka madai ya kuwa afya yake haiko katika hali nzuri.

image
na

Makala02 March 2023 - 08:41

Muhtasari


Justin Bieber  ameghairi ziara zake za Justice World Tour Dates kwa sababu za kiafya ,alisema kuwa ailemewa alipokuwa akifanya shoo zake barani Uropa mwaka uliopita  hivyo kuamua kuchukua mapumziko ili kuweka sawasawa afya yake.


Mwanamuziki wa nyimbo za RnB, Pop, Dance Pop maarufu Justin Bieber amekatiza safari zake zilizobakia za ' Justice World tour  dates' kwa sababu za kiafya. Mwimbaji huyo mwenye miaka 29 amelazimika kuahirisha safari zake mara kadhaa akiwaeleza wafuasi wake kwama msimu wa  majira yauliopita aliugua ugonjwa wa uso unaojulikana kama vile Ramsay Syndrome hivo alisema Septemba mwaka jana kuwa alitaka kushughulikia na kuipa afya yake kipaumbele .

Mwanamuziki huyo kutoka nchi ya Kanada alikuwa anatarajiwa kufanya shoo zake nchini Australia,Amerika,Bara la Ulaya,Bara Asia ikiwemo Uingereza upande wa Manchester ambayo ilikuwa ifanyike tarehe 4 Machi 2023.

Hata hivyo baadhi ya Mashabiki wake hapo awali walieleza masitiko yao kuhusu kutorudishiwa pesa zao kwa tarehe zilizoahirishwa kwenye ziara hiyo ambayo imefutiliwa mbali na ambayo imeripotiwa kuwa na kipato cha dola milioni 55. Bado hakuna sababu rasmi ya kughairiwa imetolewa.

Mwimbaji huyo ambaye ameshinda tuzo za Grammy miaka za nyuma alichukua mapumziko kutoka kwa kwa muziki mwaka wa 2019 ili kushughulkia afya ya akili yake.Alidai kuwa shoo zilizokuwa zimebakia barani Uropa zilikua zimemlemea hivyo alihitaji kupuzika.

Ugonjwa wa Ramsay Syndrome ni wakati ambapo mlipuko wa shingles huathiri mishipa ya uso karibu na masikio ya mtu na kusababisha kupooza kwa sehemu za uso,haiwezi kupitishwa kutoka kwa mtu mmoja hadi mwingine lakini hutokana na virusi vya shingles ambayo mtu anaweza kupata akiwa mtoto.

Justin Bieber anajulikana kwa wimbo kama vile Sorry, What do you mean kati ya nyinginezo.


RADIO JAMBO FREQUENCIES

Kisumu 100.1 | Mombasa 92.3 | Nakuru 96.9 | Eldoret 99.5 | Nyeri 99.3 | Nyahururu 97.3 | Webuye 95.3 | Meru 92.7 | Kitui 104.9 | Kibwezi 104.7 | Voi 105.7 | Malindi 98.1 | Lamu 104.7 | Narok 97.3 | Kapenguria 99.7 | Kisii 89.3 | Garissa 104.3 | Maralal 97.3 | Lodwar 92.7


logo© Radio Jambo 2024. All rights reserved