logo

NOW ON AIR

Listen in Live

Mammito kumpeleka 'date' mwanaume aliyekiri mapenzi kwake

Mchekeshaji Mamito amesema kuwa angependa kumpeleka date mwanaume aliyeonyesha nia ya kumuoa mamito.

image
na

Makala12 June 2023 - 09:03

Muhtasari


• Miaka ya awali kulikuwa na uvumi kuhusiana na mahusiano ya mcheshi huyo na Mcheshi mwenzake, Butita.

• Mamito akiandika kwenye akaunti yake ya Insytagram alifurahishwa na pendekezo la mwanaume huyo ambaye alisema  kuwa angependa kumuoa.

Mchekeshaji Mamito na Mwanaume anyetaka kumuoa.

Mchekeshaji Eunice Wanjiru almaarufu Mammito amesema kuwa angependa kumpeleka date mwanaume aliyeonyesha nia ya kumuoa Mammito.

Mammito akiandika kwenye akaunti yake ya Instagram alifurahishwa na pendekezo la mwanaume huyo ambaye alisema  kuwa angependa kumuoa.

“Ati kuna mtu angependa kunioa? Ako wapi? nafaa kumpeleka date” aliandika mammito

Mwanaume huyo anayefahamika kama Jokin254 Jumapili alijitokeza na kuzungumza akisema kuwa anampenda mcheshi huyo na angependa kumuoa.

“Wakenya Jina langu ni Jokins254, namtafuta Mamito Eunice awe mke wangu.” mwanaume huyo aliandika.

Jokins254 aliwasihi Wakenya wamuambie mammito ajibu jumbe zake ama ampigie kwenye namba yake aliyoandika kwenye bango.

“Mwambieni ajibu jumbe zangu ama anipigie.”

Mwanaume huyo kutoka Kinangop alisema kuwa amesafiri kutoka kaunti ya Nyandarua hadi Nairobi kwa sababu ya mapenzi yake ya dhati kwa mcheshi huyo.

Jokins pia alimhakikishia Mammito kuwa kimkubali kuwa kwenye mahusiano naye atakuwa mwaminifu na haezi watafuta wanawake wengine.

“Mammito mimi ukieza nikubali sitai kucheza na mimi mapenzi ndio nitakupea”

Mwanaume huyo pia aliwaonya wanaume dhidi ya kuzungumza na mamito kwa nia ya kuchumbiana naye na akasisitiza kuwa kama Mammito hatakuwa mpenzi wake basi hataki mwanamke mwingine.

Miaka ya awali kulikuwa na uvumi kuhusiana na mahusiano ya mcheshi huyo na Mcheshi mwenzake, Butita licha ya wawili hawa kukataa uwezekano wa kuwa na mahusiano ya kimapenzi baina yao.

Mammito aidha hajajitokeza wazi na kufichua uhusiano wake wa kimapenzi na mwanaume yeyote.

Mchekeshaji huyo pia ni mwigizaji katika vipindi kadhaa za hapa nchini na pia anafanya video fupi fupi za Tiktok akimshirikisha rafiki yake mkubwa Awinja.


RADIO JAMBO FREQUENCIES

Kisumu 100.1 | Mombasa 92.3 | Nakuru 96.9 | Eldoret 99.5 | Nyeri 99.3 | Nyahururu 97.3 | Webuye 95.3 | Meru 92.7 | Kitui 104.9 | Kibwezi 104.7 | Voi 105.7 | Malindi 98.1 | Lamu 104.7 | Narok 97.3 | Kapenguria 99.7 | Kisii 89.3 | Garissa 104.3 | Maralal 97.3 | Lodwar 92.7


logo© Radio Jambo 2024. All rights reserved