Alphonse kutoka Congo amesimulia kwa uchungu jinsi alivyojifungua mbuzi badala ya mtoto baada ya kubeba ujauzito wake kwa miezi tisa.
Kulingana naye ni kwamba alikutana na mumewe kijijini kwao wakawa wapenzi na akaolewa naye wakaanza kuishi kama mume na mke na wakajaliwa watoto 6.
Anasema kuwa alipata ujauzito wa mtoto wake wa saba na kila kitu kilikuwa sawa, muda wa kujifungua ulipofika mume wake alikuwa hayupo nyumbani na mvua ilikuwa ikinyesha hivyo mkunga wa kijijini kwao ndiye alimsaidia kujifungua nyumbani.
Alijifungua lakini safari hii hakuwa mtoto bali ni mbuzi.Mkunga hakuamini na kuwaita majirani ambao walishuhudia kuwa ni mtoto wa mbuzi na Watu wakaanza kusema ni uchawi.
Mumewe alipokuja na kumuona mtoto wa mbuzi baada ya dakika 30 alifariki na wakamzika, mumewe alimuacha na watoto sita na kusema hawezi kuishi na mtu aliyezaa mbuzi. Majirani zake nao waliacha kuongea naye na kuamua kurudi nyumbani kwa mzazi wake.