logo

NOW ON AIR

Listen in Live

Jamaa aishiwa na nguvu baada ya kupoteza 200k kwa kamari muda mfupi baada ya kushinda

Alionekana amenyong'onyea na kulala kitandani.

image
na Radio Jambo

Makala16 January 2024 - 07:48

Muhtasari


β€’ benbills007 alisema: "Hilo ni jambo moja kuhusu kamari πŸ˜‚..Utashinda, lakini siku watakapoenda kukusanya pesa zako zote, utalia siku hiyo πŸ˜‚."

Mcheza kamari

Mwanamume mmoja mwenye umri wa makamo aliishiwa na nguvu na kupoteza fahamu kwa muda baada ya kupoteza laki mbili katika mchezo wa Kamari muda mfupi tu baada ya kushinda pesa hizo kutoka kwa mchezo huo huo wa Kamari.

Kwa mujibu wa blogu ya GossipMill iliyochapisha hadithi hiyo, mwanamume huyo alibahatika kushinda mchezo wa Kamari na kupata Naira laki mbili lakini tamaa ikamuingia na kupata msukumo wa kutaka kushinda Zaidi.

Hapo ndipo alianza na kuweka kima cha Naira elfu 40 ambazo zilienda na kabla hajagutuka, akapata laki mbili zote zimeshakunywa maji ndani ya muda mfupi tu, na furaha ikageuka kuwa majonzi.

Video iliyoenea kwenye mitandao ya kijamii ilinasa wakati wa kuhuzunisha kijana alijikuta kutokana na uwekezaji wake duni, na alionekana amejilaza kwenye godoro akiwa ameishiwa na nguvu huku akiwa hataki kabisa kuiona simu yake baada ya kupoteza mpunga.

Haya hapa ni baadhi ya maoni ya watu katika chapisho hilo;

benbills007 alisema: "Hilo ni jambo moja kuhusu kamari πŸ˜‚..Utashinda, lakini siku watakapoenda kukusanya pesa zako zote, utalia siku hiyo πŸ˜‚."

 

dansky_exchange alitoa maoni: “Dau kamwe si njia ya kupata pesa…nyumba hakika itashinda…UTPOTEZA PESA YAKO.:

 

mcjblazedwfc alitoa maoni yake: "Tukikimbia Pesa sasa atakwenda bado kubeba Man U kushinda au sare πŸ˜‚πŸ˜‚πŸ˜‚."

 

king_cozzy_ alibainisha: "Pesa atatumia kununua shuka mpya πŸ˜‚πŸ˜‚πŸ˜‚πŸ˜‚."

 


RADIO JAMBO FREQUENCIES

Kisumu 100.1 | Mombasa 92.3 | Nakuru 96.9 | Eldoret 99.5 | Nyeri 99.3 | Nyahururu 97.3 | Webuye 95.3 | Meru 92.7 | Kitui 104.9 | Kibwezi 104.7 | Voi 105.7 | Malindi 98.1 | Lamu 104.7 | Narok 97.3 | Kapenguria 99.7 | Kisii 89.3 | Garissa 104.3 | Maralal 97.3 | Lodwar 92.7


logoΒ© Radio Jambo 2024. All rights reserved