logo

NOW ON AIR

Listen in Live

"Najivunia kukuzaa, kuwa Mama bora kwako" Mama Dangote amsherehekea mkubwa wa Diamond

Mama Dangote alibainisha jinsi anavyojivunia kuwa mzazi wa malkia huyo na kumtakia maisha marefu.

image
na Radio Jambo

Habari02 February 2023 - 08:39

Muhtasari


β€’"Namshukuru Mungu kwa kutimiza miaka 37 pia Nashukuru kwa kunipa MaBinti Wazuri wenye upendo," Esma alisema.

β€’ Mama Dangote alibainisha jinsi anavyojivunia kuwa mzazi wa malkia huyo na kumtakia maisha marefu.

Dada ya staa wa Bongo, Diamond Platnumz, Esma Platnumz anaadhimisha siku yake ya kuzaliwa hivi leo, Februari 2.

Esma ametoa shukrani za dhati kwa Mola kwa hatua aliyofikia huku akimuomba mafanikio zaidi katika maisha yake.

"Namshukuru Mungu kwa kutimiza miaka 37 pia Nashukuru kwa kunipa MaBinti Wazuri wenye upendo," alisema.

Mfanyibiashara huyo aliweka wazi kuwa hana majuto kwa yale aliyofanya maishani kufikia sasa anapoendelea kuzeeka.

Wakati huohuo, alidokeza kuhusu mpango wake kuongeza mtoto mwingine kufuatia shinikizo kutoka kwa binti zake.

"Nawaahidi kilio chenu cha kutaka mdogo wenu nalifanyia kazi nitazaa hata na chizi ilimradi niwafurahishe maana umri unakimbia jamani khaaa!!!… πŸ˜‚πŸ€£" alisema.

Mamia ya wanamitandao wakiwemo marafiki, wanafamilia na mashabiki wameendelea kumsherehekea Esma na kumtakia kheri ya siku ya kuzaliwa.

Mama yake, Mama Dangote ni miongoni mwa waliomwandikia jumbe nzuri za kumsherehekea kwenye mtandao wa Instagram.

Katika ujumbe wake, Mama Dangote alibainisha jinsi anavyojivunia kuwa mzazi wa malkia huyo na kumtakia maisha marefu.

"Sina cha kuandika..Ila najivunia kukuzaa na kuwa Mama bora kwako Esma πŸ₯° @_esmaplatnumz Nakutakia maisha marefu yenye baraka tele ..Kwenye kuongeza mwaka mwengine," aliandika Mamake Diamond.

Esma alijibu, "Asante sana na nimekuwa Mama bora kwa watoto wangu pia 😍"

Bila shaka, siku zote wawili hao wamekuwa na uhusiano mzuri na Mama Dangote ameonekana akimtembelea Esma katika duka lake la nguo mara nyingi na hata kumsaidia katika matangazo ya bidhaa zake.

Mzazi mwenza wa Rayvanny, Fahyma pia amemsherehekea Esma mnamo siku hiyo maalum katika maisha yake.

"Aaww, hii inapendeza sana. Kheri ya siku ya kuzaliwa mpendwa @_esmaplatnumz Nakupenda," aliandika.


RADIO JAMBO FREQUENCIES

Kisumu 100.1 | Mombasa 92.3 | Nakuru 96.9 | Eldoret 99.5 | Nyeri 99.3 | Nyahururu 97.3 | Webuye 95.3 | Meru 92.7 | Kitui 104.9 | Kibwezi 104.7 | Voi 105.7 | Malindi 98.1 | Lamu 104.7 | Narok 97.3 | Kapenguria 99.7 | Kisii 89.3 | Garissa 104.3 | Maralal 97.3 | Lodwar 92.7


logoΒ© Radio Jambo 2024. All rights reserved