logo

NOW ON AIR

Listen in Live

Zari Hassan na mpenzi wake Shakib wazika tetesi za kuachana

Wapenzi hao wawili pia walionekana wakikumbatiana na kubusu midomoni walipokuwa katika uwanja wa ndege.

image
na Radio Jambo

Makala01 February 2023 - 05:29

Muhtasari


•Wapenzi hao wawili pia walionekana wakikumbatiana na kubusu midomoni walipokuwa katika uwanja wa ndege.

•Uvumi wa kutengana ulizuka wakati wawili hao walipochapisha ujumbe wa kimafumbo kwenye mitandao ya kijamii.

Mwanasoshalaiti wa Uganda Zari Hassan amechapisha video nzuri zake na mpenzi wake Shakib Cham Lutaaya wakifurahia nyakati za kimapenzi pamoja huku kukiwa na tetesi kuwa wawili hao wamesitisha mahusiano yao ya miezi kadhaa.

Kwenye akaunti yake wa Snapchat, mzazi mwenza huyo wa staa wa Bongo Diamond Platnumz alichapisha video inayomuonyesha akimuaga Shakib ambaye alikuwa akielekea mahali pengine ambapo hawakuficha.

"Tuonane hivi karibuni. Nakupenda,"  alisikika akisema kwenye video hiyo.

Shakib vilevile alimhakikishia mama huyo wa watoto watano kuhusu mapenzi yake makubwa kwake na kumuaga kwaheri.

"Kwaheri mpenzi wangu. Nakupenda," alisema.

Wapenzi hao wawili pia walionekana wakikumbatiana na kubusu midomoni walipokuwa katika uwanja wa ndege.

Haya yanajiri huku kukiwa na uvumi kuwa penzi la wawili hao limegonga mwamba, miezi michache tu baada ya kuanza kuchumbiana.

Uvumi huo ulienea zaidi mwishoni mwa juma lililopita wakati raia hao wawili wa Uganda walipochapisha ujumbe wa kimafumbo kwenye mitandao ya kijamii.

Zari ambaye ana umri wa miaka 41 aliibua wasiwasi kuhusu mahusiano yake na kijana huyo mwenye umri wa miaka 31 baada ya kuchapisha nukuu ambayo ilielezea hatari ya uwongo miongoni mwa watu wako wa karibu.

Baadhi ya watu hawaelewi jinsi uwongo unaweza kuwa sumu. Uongo huambukiza na kulaani mahusiano yenye furaha hadi unahisi kuumwa na tumbo kwa kuwaamini tena,

Haijalishi ni kiasi gani unampenda mtu, wakati mwingine huwezi kujizuia kujisikia kama aliiba Faraja yako. Huna raha tena kwa sababu unakisia kila kitu. Sasa, kuwaamini sio kazi rahisi. Sasa inahitaji bidii na wakati mwingine hiyo inachosha ilisomeka nukuu hiyo ya Horacio Jones ambayo alichapisha kwenye Snapchat.

Siku ya Jumatatu hata hivyo, Shakib alidokeza kuwa bado ana uhusiano mkubwa na familia ya mke huyo wa zamani wa Diamond Platnumz.

Mganda huyo anayeshi Afrika Kusini alichapisha picha ya watoto  wa Zari; Pinto Tale, Tiffah Dangote na Prince Nillan na kuwaonyesha upendo watatu hao. Aliambatanisha chapisho hilo na wimbo wa Drake, Forever, kipande kinachosema, "It may not mean nothing to y'all, Understand nothin' was done for me, So I don't plan on stoppin' at all, I want this sh*t forever man, ever man, ever man I'm sellin' sh*t down at the mall

Inatafsiriwa: (Inawezekana isimaanishe chochote kwenu, Lakini elewa kwamba hakuna nilichofanyiwa, kwa hivyo sina mpango wa kuacha kabisa, nataka hili milele, milele. Nauza hili chini kwenye maduka

Pia aliambatanisha ujumbe huo na emoji ya moyo ambayo mara nyingi huashiria upendo.


RADIO JAMBO FREQUENCIES

Kisumu 100.1 | Mombasa 92.3 | Nakuru 96.9 | Eldoret 99.5 | Nyeri 99.3 | Nyahururu 97.3 | Webuye 95.3 | Meru 92.7 | Kitui 104.9 | Kibwezi 104.7 | Voi 105.7 | Malindi 98.1 | Lamu 104.7 | Narok 97.3 | Kapenguria 99.7 | Kisii 89.3 | Garissa 104.3 | Maralal 97.3 | Lodwar 92.7


logo© Radio Jambo 2024. All rights reserved