logo

NOW ON AIR

Listen in Live

Mwimbaji wa injili Mary Lincoln atubu, aombewa baada ya picha zake za uchi kusambaa mitandaoni

Lincoln aliitisha mkutano wa maombi ambapo kundi la wachungaji lilimwombea.

image
na Radio Jambo

Habari01 November 2022 - 04:03

Muhtasari


•Mary Lincoln ameungama dhambi za na kutubu baada ya picha zake chafu kusambaa kwenye mitandao ya kijamii wiki iliyopita.
•Askofu Wanderi aliomba radhi kutoka kwa Mungu na Wakenya kwa niaba ya Lincoln na kanisa lote kwa jumla.

Mwimbaji wa nyimbo za injili za Kikuyu Mary Lincoln ameungama dhambi za na kutubu baada ya picha zake chafu kusambaa kwenye mitandao ya kijamii wiki iliyopita.

Mnamo Jumatatu, Lincoln ambaye ni mke wa mtangazaji maarufu wa Kikuyu Njogu wa Njoroge aliitisha mkutano wa maombi ambapo kundi la wachungaji lilimwombea.

Mkutano huo wa maombi ambao uliofanyika katika kanisa la CFF Kiambu ulipeperushwa moja kwa moja kwenye YouTube na mitandao mingine ya kijamii. Askofu wa kanisa hilo Bishop Michael Wanderi ndiye aliongoza ibada hiyo.

"Asante Mungu kwa upendo wenu. Bishop Wanderi na Rev David Mwangi Mungu awabariki 🙏 Shiru Wa Gp Kenya ,Joyce Irungu The Bosslady, Karangu Muraya, Anne Lawrence, Judie Masila, Wairimu Muchiri na wasanii wenzangu wote na marafiki wote ambao wamekuwa wakisali nami, asanteni sana," Lincoln alisema baada ya ibada.

Wakati wa ibada, Askofu Wanderi aliomba radhi kutoka kwa Mungu na Wakenya kwa niaba ya Lincoln na kanisa lote kwa jumla.

Aliwahimiza watu kuchukua hatua za ujasiri kama vile kutubu baada ya kutenda dhambi badala ya kuchukua maisha yao.

"Hili ni kosa. Hatutalirudia tena. Tunamuomba Mungu atusamehe kama kanisa. Nasimama hapa kama askofu kuomba msamaha kwa Mungu na kwa watu wote ambao waliona zile picha..Kuna watu kadhaa katika Bibilia ambao walitenda kosa, moja alikuwa Judas. Alimsaliti Yesu lakini hakuchukua njia nzuri kama ile Mary alichukua. Sisi ambao tunajuana na Mungu , ata  lifanyike la aina gani, hatuchukui njia ya Judas," alisema.

Mwimbaji Shiru wa GP alizungumza kwa niaba ya wasanii kadhaa ambao walikuwa wamefika katika kanisa hilo kumuunga mkono Lincoln.

Wiki iliyopita baadhi ya picha za utupu zinazodaiwa kuwa za mwimbaji huyo wa nyimbo za injili zilisambaa kwenye mitandao ya kijamii.

Wakenya wengi walijitokeza kumkosoa msanii huyo na kumshutumu kwa unafiki. Hata hivyo, wengine walimtetea wakidai kwamba kila mtu ana mwelekeo wa kufanya dhambi.


RADIO JAMBO FREQUENCIES

Kisumu 100.1 | Mombasa 92.3 | Nakuru 96.9 | Eldoret 99.5 | Nyeri 99.3 | Nyahururu 97.3 | Webuye 95.3 | Meru 92.7 | Kitui 104.9 | Kibwezi 104.7 | Voi 105.7 | Malindi 98.1 | Lamu 104.7 | Narok 97.3 | Kapenguria 99.7 | Kisii 89.3 | Garissa 104.3 | Maralal 97.3 | Lodwar 92.7


logo© Radio Jambo 2024. All rights reserved