logo

NOW ON AIR

Listen in Live

"Nguvu ipo kabisa!" DJ Mo afichua faida za Size 8 kuomba kabla ya kushiriki mapenzi

"Utaweza kuelewa katiba vizuri zaidi kwa angalau saa moja," alisema.

image
na Radio Jambo

Habari28 March 2023 - 05:29

Muhtasari


•Mo alidokeza kwamba kusali kabla ya kuzamia kwenye tendo humsaidia mwanamume kuonyesha umahiri kwa muda mrefu zaidi.

•Size 8 aliweka wazi kwamba huwa anaomba mumewe aweze kumridhisha ili asiwahi kupatwa na fikra za kuenda nje ya ndoa.

Mwimbaji huyo amezindua kanisa lake.

Mcheza Santuri mashuhuri Samuel Muraya almaarufu DJ Mo amesisitiza kuwa ni muhimu kwa wanandoa kusali kabla ya kushiriki tendo la ndoa.

Akizungumza kwenye ukurasa wake wa Instagram siku ya Jumatatu, baba huyo wa watoto wawili alidokeza kwamba kusali kabla ya kuzamia kwenye tendo humsaidia mwanamume kuonyesha umahiri kwa muda mrefu zaidi.

"Kuomba ni muhimu sana, haswa kimoyomoyo, kama unajua unajua," alisema.

Aliongeza, "Utaweza kuelewa katiba vizuri zaidi kwa angalau saa moja."

DJ Mo pia alidokeza kwamba maombi kabla ya mapenzi humsaidia mwanaume kuwa na nguvu ya kushiriki katika tendo hilo.

Haya yanajiri siku chache tu baada ya mkewe, Size 8 kufichua kwamba huwa anaomba kabla ya wao kushiriki tendo la ndoa.

Akizungumza kwenye chaneli ya YouTube ya Diana Chacha, mama huyo wa watoto wawili alifichua kwamba anaomba ili apate hamu ya kufanya mapenzi wakati  mumewe anapotaka lakini hajisikii tayari.

Mwimbaji huyo wa nyimbo za injili pia alifichua kwamba kabla ya kuzamia kwenye mchezo huo wa kitandani, yeye kawaida humwombea mumewe DJ Mo apate nguvu za kumridhisha kama ambavyo angetaka.

"Akikuja huwa namshika nasema 'Baba katika jina la Yesu' (Huwa hajui). Huwa naambia Mungu ampatie nguvu nataka kujibamba," alisema.

Mhubiri huyo alibainisha kuwa huwa anafanya maombi hayo bila ya mumewe kujua.

"Huwa naomba kimoyomoyo namwambia Mungu ,' Mungu Baba patia huyu mwanaume nguvu, wewe ndiye uliumba tendo hili, Baba jinsi ulivyoliumba,nataka kulifurahia jinsi ambavyo uliona," alisema.

Size 8 aliweka wazi kwamba huwa anaomba mumewe aweze kumridhisha ili asiwahi kupatwa na fikra za kuenda nje ya ndoa.

DJ Mo kwa upande wake alisema wakati akielekea nyumbani, pia yeye hufanya ombi kwa Mungu akimsihi awape kipindi kizuri.

"Wakati akiomba na mimi nikiwa kwa gari huwa nasema atajua mimi ni nani," alisema.

Wanandoa hao waliwashauri wapenzi wengine kumshirikisha Mungu kila wakati wanaposhiriki tendo la ndoa.

"Watu hucheka wakiambiwa ati waombe kabla ya mapenzi. Yeye (DJ Mo) hajui, lakini mimi kwa upande wangu huomba," alisema.


RADIO JAMBO FREQUENCIES

Kisumu 100.1 | Mombasa 92.3 | Nakuru 96.9 | Eldoret 99.5 | Nyeri 99.3 | Nyahururu 97.3 | Webuye 95.3 | Meru 92.7 | Kitui 104.9 | Kibwezi 104.7 | Voi 105.7 | Malindi 98.1 | Lamu 104.7 | Narok 97.3 | Kapenguria 99.7 | Kisii 89.3 | Garissa 104.3 | Maralal 97.3 | Lodwar 92.7


logo© Radio Jambo 2024. All rights reserved