logo

NOW ON AIR

Listen in Live

Stephen Letoo ataka Mfalme Charles kushiriki kikao na wajumbe wa Men's Conference, fahamu kwa nini

“Tungependa kujadiliana na mfalme kuhusu masuala ya maslahi ya pande zote, tunatumai shughuli nyingi za mfalme zitaturuhusu kukutana naye," Letoo alisema.

image
na Radio Jambo

Habari31 October 2023 - 04:22

Muhtasari


•Letoo ameandika barua kwa Ubalozi wa Uingereza jijini Nairobi akiwakaribisha Mfalme Charles III wa Edinburg na Malkia Camilla nchini Kenya.

•Ameomba wajumbe wa Men’s Conference watengewe muda na Mfalme Charles akipendekeza kuwa majadiliano yatakuwa kuhusu masuala ya maslahi ya pande zote.

ameomba kukutana na King Charles III

Mwanahabari maarufu wa Kenya, Stephen Letoo, ambaye pia ni mwenyekiti wa kujitangaza wa Mpango wa Men’s Conference ameandika barua kwa Ubalozi wa Uingereza jijini Nairobi akiwakaribisha Mfalme Charles III wa Edinburg na Malkia Camilla nchini Kenya.

Wawili hao wa familia ya Kifalme ya Uingereza waliwasili Kenya siku ya Jumatatu usiku na wakakaribishwa na Waziri Mkuu Musalia Mudavadi na Balozi wa Uingereza nchini Kenya, Neil Wigan.

Katika barua yake kwa Ubalozi wa Uingereza, mwanahabari huyo wa Citizen TV pia ametoa ombi maalum kwa mfalme Charles III kushiriki kikao na wajumbe wa mkutano wa wanaume (men’s conference).

"Mpango wa mkutano wa wanaume (men’s conference) ni mkusanyiko wa wanaume kutoka nyanja zote za maisha, ambao wamejitolea kwa ukuaji wa kibinafsi, uongozi, mabadiliko ya hali ya hewa, kutokomeza umaskini na kujenga jamii. Dhamira yetu ni kumwezesha mwanaume kuwa bora zaidi kupitia mseto wa wazungumzaji wakuu wa kusisimua, warsha zinazoshirikisha na fursa za mitandao,” Letoo aliandikia Ubalozi Mkuu wa Uingereza.

Aliendelea, “Tunaomba rasmi kuwa na mazungumzo baina ya pande mbili na wajumbe wake Mfalme Charles tunapotarajia kushiriki mipango yetu; ufahamu wa afya ya akili, uwezeshaji wa wanawake, matumizi mabaya ya dawa za kulevya na mabadiliko ya hali ya hewa."

Letoo aliendelea kuomba wajumbe wa Men’s Conference watengewe muda na Mfalme Charles akipendekeza kuwa majadiliano yatakuwa kuhusu masuala ya maslahi ya pande zote.

“Tungependa kujadiliana na mfalme kuhusu masuala ya maslahi ya pande zote, tunatumai kuwa shughuli nyingi za mfalme zitaturuhusu kukutana naye. Asante kwa kuzingatia kwako na tunatarajia kusikia kutoka afisi yako,” aliandika.

Ndege ya Kifalme ya Uingereza ambayo ilikuwa imewabeba Mfalme Charles III na Malkia ilifika katika Uwanja wa Ndege wa Kimataifa wa Jomo Kenyatta (JKIA) dakika chache kabla ya saa tano Jumatatu usiku. Wawili hao wako nchini Kenya kwa ziara ya kiserikali ya siku nne itakayoanza rasmi Jumanne, Oktoba 31.

Ziara hiyo inalenga kusherehekea uhusiano mzuri baina ya nchi hizo mbili na ushirikiano thabiti na mahiri wanaoendelea kuuanzisha.

Mfalme na Malkia watazuru Kaunti ya Jiji la Nairobi, Kaunti ya Mombasa, na maeneo jirani.


RADIO JAMBO FREQUENCIES

Kisumu 100.1 | Mombasa 92.3 | Nakuru 96.9 | Eldoret 99.5 | Nyeri 99.3 | Nyahururu 97.3 | Webuye 95.3 | Meru 92.7 | Kitui 104.9 | Kibwezi 104.7 | Voi 105.7 | Malindi 98.1 | Lamu 104.7 | Narok 97.3 | Kapenguria 99.7 | Kisii 89.3 | Garissa 104.3 | Maralal 97.3 | Lodwar 92.7


logo© Radio Jambo 2024. All rights reserved