Programu ya kimataifa ya kusambaza chakula ya Uber Eats imeungana na wasambazaji wa bidhaa jijini Toronto, Canada, kutoa huduma za kusambaza Bangi kwa wenyeji.
Leafly, ambayo ni biashara ya kuanzisha, ndiye mshirika rasmi wa huduma hiyo ambayo itango'a nanga siku ya Jumatatu.
Duka hilo ambalo liko katika jiji la Seattle, takriban kilomita 160 kusini mwa mpaka wa Canada linatoa huduma za kuuza bangi mitandaoni.
Wanasema ushirikiano huo utasaidia kukabiliana na soko haramu la chinichini ambalo wanasema linajumuisha zaidi ya asilimia 50 ya mauzo ya bangi zisizo za kimatibabu.
"Kwanza kabisa, tunaona hii kama sehemu muhimu ya kukomesha kuendesha gari chini ya shinikizo, na pili, huu ni mpango mwingine tu ambao unaweza kusaidia kupambana na soko haramu la bangi, ambalo bado linaunda zaidi ya asilimia 40 ya mauzo ya bangi jijini Ontario leo," Meneja mkuu wa Uber Eats nchini Canada Lola Kassim alisema.
Huduma hiyo itapatikana kwa watu wazima wenye umri wa miaka 19 na zaidi.
Watu wanaruhusiwa kuagiza na kuwa na hadi gramu 30 pekee za bangi halali.
Mchakato wa kuagiza bangi utakuwa na mchakato wa kuagiza chakula, lakini bangi itawasilishwa tu na wafanyikazi walioidhinishwa na serikali na duka hilo na wala si tu dereva mwingine yeyote wa Uber Eats.
Mfanyikazi lazima athibitishe umri na usawa wa mteja anapowasili.
Mnamo Oktoba 17, 2018, bangi ilihalalishwa nchini Canada kwa madhumuni ya burudani na matibabu. Ilikuwa tayari halali kwa madhumuni ya matibabu, chini ya hali fulani.