logo

NOW ON AIR

Listen in Live

Utafiti 'tata' wa mayai ya uzazi yanayotengenezwa kwa seli za kiume za panya

Mtafiti wa Kijapan amesema kuwa ameweza kutengeneza mayai ya uzazi kwa kutumia seli za kiume za panya

image
na Radio Jambo

Habari13 March 2023 - 03:46

Muhtasari


•Mtafiti wa Kijapan amesema kuwa ameweza kutengeneza mayai ya uzazi kwa kutumia seli za kiume za panya.

•Profesa George Daley wa Chuo kikuu cha tiba cha Harvard Medical alisema kuwa bado utafiti huu una safari ndefu kabla ya jamii kukubali uamuzi wa aina hiyo.

Mtafiti wa Kijapan amesema kuwa ameweza kutengeneza mayai ya uzazi kwa kutumia seli za kiume za panya.Hayash ameyasema hayo katika mkutano wa kimataifa kuhusu jeni za urithi mjini London..

Utafiti huo ambao uko katika hatua zake za mwanzo, unahusisha kubadili kile kinachoitwa kisayansi jinsia ya XY Kromosomu ( XY sex chromosomes) kutoka kuwa ya kiume na kuwa ya kike au kutoka kwa mayai ya uzazi ya kike.

Profesa Katsuhiko Hayashi kutoka chuo kikuu cha Osaka nchini Japan anasema anaendelea na juhudi za kutengeneza tiba ya kutokuwa na uwezo wa kuzaa au kuzalisha.

Taarifa ya utafiti huu ambayo imechapishwa kwenye jarida la masuala ya kisayansi Nature, imeibua mjadala huku wengi wakisema kuwaiwapo utafiti huu utakuwa na ufanisi kuna uwezekano wa "wanaume wanaoshiriki mapenzi ya jinsia moja" wa jamii ya LGBTQ wanaweza kuwa na watoto kwa njia hiyo.

Profesa George Daley wa Chuo kikuu cha tiba cha Harvard Medical , ambaye hakuhusika katika utafiti huu, alisema kuwa bado utafiti huu una safari ndefu kabla ya jamii kukubali uamuzi wa aina hiyo.

"Kazi ya Katsuhiko Hayashi haijachapishwa lakini ni ya kufurahisha. Itakuwa vigumu kuwafanya watu kama panya," alisema. Hatujaelewa bado kuhusu baiolojia ya seli za binadamu(kuhusu uundwaji wa tishu za uzazi) iwapo zinaweza kutengenezwa saw ana kazi ya Hayashi katika panya .''

Maelezo ya utafiti huu yaliwasilishwa katika mkutano wa uhariri wa jeni za binadamu uliofanyika katika taasisi ya Crick mjini London.


RADIO JAMBO FREQUENCIES

Kisumu 100.1 | Mombasa 92.3 | Nakuru 96.9 | Eldoret 99.5 | Nyeri 99.3 | Nyahururu 97.3 | Webuye 95.3 | Meru 92.7 | Kitui 104.9 | Kibwezi 104.7 | Voi 105.7 | Malindi 98.1 | Lamu 104.7 | Narok 97.3 | Kapenguria 99.7 | Kisii 89.3 | Garissa 104.3 | Maralal 97.3 | Lodwar 92.7


logo© Radio Jambo 2024. All rights reserved